Hili swali labda ungeuliza "nyumba ya kisasa lazima iweje", kidogo hapo ningejua nikueleze nini lakini ukubwa wa nyumba hauhusiani na usasa.
Ukubwa wa nyumba inategemea na mfuko wako na mahi mahi yako. Wapi wanaosema nyumba ndogo km vyumba 3 ni rahisi kuitunza lakini kubwa watoto wakiitwa linabaki gofu. Kwa mtazamo wangu mtu km huyu yupo sahihi kwa mahitaji yake na kipato chake. Hakuna mwanadamu asiyependa vitu vizuri na vikubwa. Mfano ukipewa TV inchi 32 na inchi 60 itachagua ipo. Utakayochagua ndo inalingana na mahitaji yako hata gharama za matengenezo ikiharibika.
Pia ukubwa wa nyumba yako itategemea ukubwa wa familia yako. Kibongobongo waliowengi ni extended families (baba, mama, watoto, na ndugu na jamaa). Hapa ukiwa na vyumba 2 itskuwaje.
Pia ukubwa wa NYUMBA yako itategemeana na uhusiano na ndugu zako. Km umeamua kuishi maisha ya peke yako hutaki wageni wa kulala hata chumba kimoja kinakutosha. Kiimami wageni ni baraka. Unaweza kukuta kwa siku umetembelewa na wageni wa kulala wasiopungua 2 tena jinsia 2 na una watoto wa kike na kiume. Hapo vyumba 3 itakuwaje. Au ndo utamwambia mgeni alale na wanao.
Pia inategemeana na sehemu unayojenga. Mfano kuna wengine wakijenga Dar kupata wageni wa kulala ni baada ya miaka kadhaa lakini wengine kwa vile kajenga Dar kila anaekuja lazima afikie kwake. Au mtu ukijenga kijijni hiyo nyumba yako ya kisasa ya vyumba 3 unadhani utapata wageni wengi km mjini. Vilevile ukiwa umejenga NYUMBA kwenye mji ambayo huduma za binadamu km afya zinapatikana lazima ujiandae kipokea wageni wakutosha kutoka kijijini maana kwako ndo itakuwa sehemu ya kufikia (hapa inategemeana na mahusiano mliyonayo, km hutaki wageni wakiskia hawajui). Mfano mimi niliamua kujenga nyumba kubwa sababu kuu ikiwa ni hii, ndugu wakija mjini kutibiwa au kufanya shughuli zao za muda mfupi basi wapate kulala kwa amani. Na haya ndo maisha ya Kitz na ukarim ni mila na desturi zetu. Ingawa watu wasiofahamu asili yangu hushangaa kujenga nyumba km hiyo.
Haya maisha ya hapa duniani ni mafupi sana, ukiwa na uwezo wa kuupa furaha moyo wako Fanya bila kujali wengine watasemaj maana kila mtu ana maono na matamanio ktk maisha yake, hivyo hatuwezi kufanana.