Nyumba ya "watu"

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2017
Posts
10,559
Reaction score
19,101
Siku hizi nyumba kama hizi sio nyingi sana kwenye jamii yetu, nadhani inatokana na mabadiliko ya kimaisha, kijamii na pia kiuchumi
Hizi ni nyumba ambazo ndani hake wamelelewa watu wengi sana. Sio lazima watu hao wawe wanafamilia wenye mahusiano ya damu na wenye nyumba

Katika nyumba hizi siku zote hukosi watu kwa maana ya wageni wanaofikia hapo kukaa kwa muda mfupi au mrefu, au hata majirani na marafiki wa wanafamilia. Utakuta kuna majirani ambao watoto wao hushinda hapo na wakati mwingine huhamia kabisa, kuna marafiki wa wanafamilia nao hawakosekani

Maranyingi nyumba hizi sio kama zina wenyenyumba (babab na mama) wenye vipato vikubwa bali ni vya kawaida tu lakini ajabu riziki hua hazikosekani japo kwa kiasi. Nyumba huwa na furaha wakati wote na watu wanaopitia katika nyumba hizo hujenga urafiki na kua kama ndugu hadi kwenye utu uzima wao

Binafsi nimelelewa katika nyumba ya namna hiyo ambapo kuna wakati tulikua kama watu 25/30 tukiwemo watoto, ndugu, jamaa, majirani na marafiki na wafanyakazi, sote tukisoma, kucheza, na kusaidiana kazi za nyumbani za mifugo na shamba pamoja. Sasa hivi tumetawanyika na wote wanamaisha yao lakini popote tukikutana hakikika hua ni zaidi ya udugu

Sifa kuu za viongozi wa nyumba hizi (baba na mama) hua ni watu wenye upendo, wasio na undani(yaani hawana usiri wa kusengenya), sio wabinafsi wa kuwapendelea watoto wao, ni wakarimu sana. Kwa ujumla ni viongozi kwa kuzaliwa

Miaka ya nyuma kabila la Wamanyema walikua ni watu wenye sifa ya namna hii. Hili ni kabila ambalo lilikua na sifa ya kuchukulia watoto wote wanalelewa na jamii wakifunzwa adabu, heshima na utu. Popote wakutanapo watu hawa huwa ni kaka yangu na dada yangu. Lakini sina hakika kama bado wanaliendeleza hili
 
Asalam alykum mwana ndugu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…