Nyumba ya Wazanaki yanogesha maonesho ya 77 ya mwaka 2023

Nyumba ya Wazanaki yanogesha maonesho ya 77 ya mwaka 2023

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
Na. Sixmund J. Begashe

Nyumba ya asili ya kabila la Wazanaki iliyojengwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Taasisi yake ya Makumbusho ya Taifa, imekuwa kivutio kikubwa kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam Maarufu kama Saba Saba.

Makundi Makubwa ya wanaofika katika Maonesho hayo ya Kimataifa licha ya kupata huduma zingine kwenye Banda la Maliasili na Utalii, wametembelea Nyumba hiyo na kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu Kabila la Wazanaki lenye historia kubwa kupitia Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere.

Mhifadhi Mila Mwandamizi wa Makumbusho ya Taifa Bi. Flora Vincent asema kuwa sababu ya kuwa na Onesho la Nyumba ya asili kwenye Maonesho hayo makubwa ni kuipa fursa jamii kujifunza Umuhimu wa kurithisha kizazi kilichopo Mila na Desturi za Makabila mbalimbali ili kuimarisha Mshikamano wa Kitaifa, Umoja, Upendo, amani Kwa maendeleo endelevu nchini.

Akizungumzia maonesho hayo, Bibi Debora Danishashe amesema ameamua kuwaleta wajukuu zake kwenye Nyumba hiyo ili wapate uwelewa juu ya Urithi wa Utamaduni, wa makabila mbalimbali ya Tanzania.

Bibi Danishashe ameongeza kuwa, kizazi cha Leo, kimetawaliwa na ulimwengu wa utandawazi unawafanya waige tamaduni za nje na kusahau zao hivyo ubunifu uliofanywa na Wizara ya Maliasili ya kuwarithisha watu hasa watoto Utamaduni wa Kitanzania ni jambo jema la lakupongezwa sana.

Katika nyumba hiyo ya asili ya wazanaki watu wamepata kujifunza kucheza bao, kukumbushwa maadili, aina za vya kula,mavazi ya asili na jinsi ya kuhifadhi mazao kiasili
IMG-20230701-WA0007.jpg
IMG-20230701-WA0009.jpg
IMG-20230701-WA0005.jpg
IMG-20230701-WA0010.jpg
IMG-20230701-WA0011.jpg
IMG-20230701-WA0006.jpg
IMG-20230701-WA0008.jpg
 
Hizo ni nyumba za maenyesho tu siku hivi, kwa ulimwengu huu, hakuna mtu anatamani kuishi kwenye mazingira hayo. Na ukikuta kuna mtu anaishi kwenye mazingira hayo atakuwa ni mzee sana au fukara ambayo naye anatafakari ni lini ataachana na maosha hayo.
 
Tatizo la nyumba za nyasi, usiwe na adui yeyote yule mtaani kwako. Maana akiwasha kibiriti tu hizo nyasi, basi utatafuta pa kutokea.
 
Usipodilika wakati utakubadilisha dunia ya sasa kutaka watu wabaki walipotoka sio rahisi hivyo.

Ishi kulingana na wakati na mazingira
 
Hizo ni nyumba za maenyesho tu siku hivi, kwa ulimwengu huu, hakuna mtu anatamani kuishi kwenye mazingira hayo. Na ukikuta kuna mtu anaishi kwenye mazingira hayo atakuwa ni mzee sana au fukara ambayo naye anatafakari ni lini ataachana na maosha hayo.
Kuna hotel za kitalii za hivyo Bei mbaya kwa siku kulala
 
Ishu ni pale tutakapoambiwa "mpaka kukamilika kwake nyumba hiyo imegharimu takribani shillingi millioni 600 za kitanzania"
 
Back
Top Bottom