Nyumba za Dar es Salaam ya 1950s

Nyumba za Dar es Salaam ya 1950s

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
NYUMBA ZILIZOKUWAKO DAR ES SALAAM YA 1950s

Hapo chini ni mfano wa nyumba nyingi zilizokuwapo Dar-es-Salaam miaka ya 1950.

Nyumba hizi zilikuwa na vyumba sita vyumba vitatu kila upande vikiangaliana na katikati kulikuwa na ukumbi mrefu.

Uani kulikuwa na mabanda madogo jiko, vyoo na bafu.

Nyumba nyingi zilikuwa na karo ambalo lilitumika kama mahali pa kuoshea vyombo au kufua nguo.

Nyingi ya nyumba hizi zilikuwa za kupangisha kwa hiyo utakuta nyumba moja ikikaliwa na familia tofauti.

Baadhi ya nyumba zilikuwa na baraza mbele kwa ajili ya wakazi kukaa na kupumzika hasa wanaume mfano wa hiyo nyumba picha ya pili.

Wanawake kwa kawaida wao wakipumzika uani au ukumbini.

Nyumba hizi zimetoweka Kariakoo lakini nimebahatika kuziona nyumba hizi Magomeni Mapipa.

329043449_570871134958757_8510450358729476933_n.jpg
330397701_950621019634136_786916605721997984_n.jpg
 
Wazee wa Zamani hawakuzingatia Parking. Wao Kiwanja waliziba mbele chooote ndio wanakaa wao uani wanaweka Mabanda ya Wapangaji.

Hapo Magomeni Mapipa waliezeka kwa kutumia Mabati ya mapipa yaliyokuwa tupu baada ya lami kutumika toka KAJIMA aliyeweka lami maeneo hayo.

All in all nyumba za Udongo zinadumu sana kuliko hizi tofali 50 kwa mfuko wa Cement
 
Zipo sana Temeke. Wafanyakazi wengi wa viwandani na serikali (ngazi za chini) tangu enzi za mkoloni waliishi mitaa hiyo.
 
Back
Top Bottom