Nyumba za kupanga na adha zake

Nyumba za kupanga na adha zake

Santieli

Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
57
Reaction score
75
Wakuu walahi mtu unaweza tamani upate walau pesa ya shortcut ili uweze kununua au kujenga banda lako mwenyewe ka kujiegesha ili kuepukana na changamoto za nyumba za kupanga

Mafano Mimi nimepanga nyumba moja hivi, gharama yake kwa mwezi sio kubwa ni kawaida. Nikaamua niwe muungwana nikamwambia mama mwenye nyumba, "maji na umeme nitalipa" akafurahi na kuridhia.

Nina miaka miwili sasa yeye mara nyingi alikua hashindi nyumbani maana alikua matron shule moja ya mission kwa hiyo kaa yake pale nyumbani ilikua likizo ya mwezi wa sita au 12

Kodi nalipa miezi mitatu mitatu na sicheleweshi

Hivi karibuni kafukuzwa kazi kutokana na kutokua na mahusiano mazuri na wanafunzi shuleni.... Sasa kimbembe kimemkuta mke wangu pale home

1) Mke akiamka akimsalimia mama mwenye nyumba haitiki sikunyingine aitike sauti ya chini

2) Watoto wake wakikaa na mke wangu ananuna hadi kwa watoto wake hata wiki mbili

3) Mtoto wangu siku nyingine amtolee mimacho ya kuogofya ili kumtisha mtoto asiingie ndani kwake ila nikiwepo na akajua anajifanya kumpenda na kumuitaita....

4) kumbambikiza chuki mke wangu kwa majirani lakini majirani hawaoni ubaya wake wanakuja kumuambia mke wangu yoyote aliyosema


Aisee ni mengi yaani mlio na vibanda au nyumba zenu hongereni, ila sisi wengine ambao bado nadhani tutamaliza nyumba kwa kuhamahama....

Wale wa nyumba za mfukoni kama mimi mnaishije?

Nokia kitochi
 
Pole sana. Kama una kiwanja jitahidi ujenge angalau room mbili kwanza.

Sent using Jamii Forums mobile app
Duuh asante mkuu.. ila kiwanja chenyewe bado mkuu...
Nilikuja na uzi humu kuwa nina mtaji wa 2Mil nifanye biashara ipi Mods wakaunganisha uzi wangu na mwingine mwisho kukosa wachangiaji na mimi kukosa msaada wa mawazo

Nokia kitochi
 
Wakuu walahi mtu unaweza tamani upate walau pesa ya shortcut ili uweze kununua au kujenga banda lako mwenyewe ka kujiegesha ili kuepukana na changamoto za nyumba za kupanga....

Mafano mimi nimepanga nyumba moja hivi, gharama yake kwa mwezi sio kubwa ni kawaida. Nikaamua niwe muungwana nikamwambia mama mwenye nyumba, "maji na umeme nitalipa" akafurahi na kuridhia.Nina miaka miwili sasa yeye mara nyingi alikua hashindi nyumbani maana alikua matron shule moja ya mission kwa hiyo kaa yake pale nyumbani ilikua likizo ya mwezi wa sita au 12...

Kodi nalipa miezi mitatu mitatu na sicheleweshi

Hivi karibuni kafukuzwa kazi kutokana na kutokua na mahusiano mazuri na wanafunzi shuleni.... Sasa kimbembe kimemkuta mke wangu pale home..
.1) Mke akiamka akimsalimia mama mwenye nyumba haitiki sikunyingine aitike sauti ya chini....
2) watoto wake wakikaa na mke wangu ananuna hadi kwa watoto wake hata wiki mbili ..
3) Mtoto wangu siku nyingine amtolee mimacho ya kuogofya ili kumtisha mtoto asiingie ndani kwake ila nikiwepo na akajua anajifanya kumpenda na kumuitaita....

4) kumbambikiza chuki mke wangu kwa majirani lakini majirani hawaoni ubaya wake wanakuja kumuambia mke wangu yoyote aliyosema.....


Aisee ni mengi yaani mlio na vibanda au nyumba zenu hongereni, ila sisi wengine ambao bado nadhani tutamaliza nyumba kwa kuhamahama....

Wale wa nyumba za mfukoni kama mimi mnaishije?

Nokia kitochi
Pambana ujenge yako bro utakuwa na amani sana.
 
Santieli hii tabia ya wenye nyumba au wapangaji kumsalimia nakuitikia kwa sauti ya chini ama asiitikie kabisa chakufanya nikuacha kumsalimia kiumbe yeyote ukiamka asubuhi lazima watanyooka tu maana tabia hiyo imekuwa sugu kwenye nyumba nyingi sana


Sent using IPhone X
 
Wanawake hawachelewagi kuvurugana kwa Visa visivyo na kichwa Wala miguu.

Utakuta,
Huyu kamsuta JIRAN YAKE, Yule KANUNUNA,
uyu kamnyima yule chumvi- YULE KANUNA
Uyu kampita bila kumsalimia,YULE KANUNA
Uyu kavaa dela JIPYA, YULE KANUNA

hayo matatizo huwez kuyakuta kwny nyumba WANAYOISHI WANAUME TUPU.

Kikubwa,
Zichukulie kawaida. Ukitaka kuziondoa hizi changamoto.

Mtafutie kazi mkeo atoke pale nyumbani,kurudi Ni usiku.

Utaepuka migogoro isiyo na kichwa Wala miguu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani hata km utajenga room moja ni kwako!hakuna raha unayoipata moyoni kama kuwa na kwako!.pole... We anza kutafuta kiwanja cha bei ya chini kisha anza kujenga mdogo mdogo au pandisha room moja uhamie!
 
Back
Top Bottom