duh karateka pole sana wa kunyumba! Hata baba yangu alitaka kumkatalia dada yangu alipoleta mchumba jina lake lilifanania sana na wahaya lkn yeye ni muha wa kigoma, cha kushangaza aliwahi mwambia hata kaka yetu mkubwa kwamba hataki aoe mwanamke wa kihaya. Hapohapo dingi mdogo mkewe ni mhaya, mtoto wake wa mwisho wa kike aliishi sana bukoba mpaka alipomaliza std seven so ana lafudhi ya kihaya kabsaa shule hajamaliza kufukuzana na suruali tu sinza. Baba aliwahi fanya kazi karagwe labda alikuwa na sababu zake sijajua. Mimi nawafahamu wasichana wa kihaya wengi tu tena wako very decent na wamekuwa wake wazuri tu. Hii generation yetu kabila wala si sababu, sababu kubwa ni malezi mtu aliyoyapata toka kwa wazazi, pili uchumi au kipato tatu ndoto na tamaa ya kuwa na mafanikio bila kuwa na kipato cha kutosha, so kuepukana na yote hayo kijana piga shule ukipata kazi jikusanye atleast 5 yrs ndio uoe ukiwa umejiandaa kutunza mke! Pole sana wakunyumba