NYUMBANI
Ilikuwa saa saba mchana , jumatatu ya tarehe kumi mwezi wa kumi na mbili mwaka elfu mbili na arobaini na tano, Ilisomeka hivyo kwenye saa ya kidigitali iliyotoa mwanga ulioelea hewani ambao ndio ulioonyesha saa na tarehe ya siku ile .Ilikuwa imewekwa juu ya meza pembeni kidogo ya mahali ambapo Asim alikuwa bize kutengeneza mtambo wake.Ni dhahiri kuwa alikuwa akiutengeneza mtambo ule kwa muda sasa, kwani kijasho chemba kilichochirizika kutokea kwenye paji la uso mpaka mdomoni kwake kupitia shavuni kilisisitiza hilo.Macho yake ang’avu, mapana na yenye umakini makubwa licha ya uchovu aliokuwa nao yalionyesha wazi umuhimu wa ule mtambo kwani aliendelea kujilazimisha kuumaliza ule mtambo bila kujali kuchoka .
Hata hivyo alikuwa karibu kumaliza ,ilibakia nati moja tu ambayo alikuwa tayari kashaanza kuizungusha kuingia kwenye tundu lililokuwa kwenye ubao wa mtambo wake uliosheheni vipuli na nyaya nyingi za umeme. Alipomaliza kuifunga ile nati,haraka aliweka bisibisi pembeni na kukamata swichi iliyounganisha ule mtambo na chanzo cha umeme.
Alipobonyeza ile swichi mtambo mzima ulimetameta kwa taa za rangi mbali mbali , ghafla kabla hajabonyeza kitufe chekundu juu ya mtambo wake ambacho alitakiwa kukibonyeza baada ya kuwasha kulitokea mlipuko mkubwa uliotoa moto na sauti kubwa yenye kushtua ambao ulifanya vipuli vingi vilivyokuwa juu ya ubao wa ule mtambo kuruka huku na kule.
Asimu ambaye kwa sasa alikuwa tayari amerembwa na make up nzito ya masizi alibaki ameduwaa bila kujua cha kufanya kwani matarajio yote aliyokuwa nayo juu ya ule mtambo yalipotelea hewani kama mvuke wa chai. Aliusukuma ule mtambo na ulidondoka chini moja kwa moja , hakujali lile na aliinuka na kuelekea mlangoni ambapo aliitungua barakoa kubwa kisha kuivaa na kutoka nje bila kurudishia mlango. Hatua zake zilisikika kwa sauti licha ya kutembea taratibu kana kwamba alikuwa akikanyaga zege zililokomaa haswa. Alijongea mpaka lilipokuwa lundo la takataka zenye asili ya chuma ambazo zilikuwa ni sehemu za mitambo iliyoharibika na alipanda juu yake.
Eneo lile lililokuwa kama jangwa la zege likuwa halina hata dalili ya mmea wowote na anga lake lilikuwa jeusi, lilikuwa ni eneo kubwa na tupu sana na vibanda walivyoishi watu vilijengwa mbali mbali bila mpangilio.Mara zote Asim alipotoka nje na kusimama juu ya lile lundo la taka alikuwa akibubujikwa na machozi kwani kumbukumbu pekee zilizokuja kichwani mwake ni za siku ambayo hatoweza kuisahau kabisa .
Ilikuwa ni siku aliyopoteza kila kitu maishani mwake , marafiki na majirani wengi waliuawa na wavamizi kutoka dunia ya juu au mwezi mweusi kama wanavyouita. Ilimuuma Zaidi kwani hata mama yake alchukuliwa na wavamizi wale na kwenda nao huko juu mbali nje ya ulimwengu kipindi yeye alikuwa na miaka saba tu. Hakuwahi kumuona mama yake tena hadi sasa ametimiza takribani miaka ishirini na mbili.
Alipokuwa amesimama pale juu alivua ile barakoa iliyofunika uso wake wote na kutazama juu kama alivyofanyaga siku zote, na chozi moja lilidondoka kutoka kwenye jicho lake mpaka chini kwenye kioo kilichokuwa kama kimefukiwa na udongo.
Kioo kile kilipodondokewa na chozi kilitoa mwanga wa bluu na kisha kuzimika, lakini Asim hakuona chochote kwani alikuwa anatazama juu wakati ule. Uso wake ulikuwa ushaanza kuwa mwekundu kutokana na gesi chafu na kemikali iliyokuwa imetapakaa eneo zima kitu ambacho kilimlazimu kuvaa barakoa haraka kwani isingechukua hata dakika moja kabla uso wake wote kubabuka.
Alipovaa alishuka chini kutoka kwenye lile lundo na kugeuka nyuma ili arudi ndani ya kibanda chake kwani nje hapakuwa salama kukaa kwa muda mrefu, lakini kabla ya kupiga hatua nyingine alisikia sauti ya kitu kilichokuwa kama kinafufuka kutoka chini nyuma ya lile lundo na aligeuka haraka na kuona roboti aliyekuwa na udongo juu yake ambayo sasa alikuwa anasogea alipo yeye. Roboti yule aliyekuwa na umbo la mtu alisogea mpaka alipokuwa Asim na kusimama mbele yake .Asimu aliduwaa akimshangaa yule roboti
Roboti: Habari ninaitwa……..itwa…….ii……iiit…….iiii….itw
Asimu alimpiga kidogo kichwani baada ya kuona inakwama kwama na kuendelea kumtazama baada ya kufanya hivyo
Roboti: Habari naitwa Rex nimetoka kwenye mwezi mweusi kuja kukuletea ujumbe , je wewe ni Asimu?
Asimu:Hapana umekosea sio mimi
Asimu alimwambia yule roboti na kugeuka nyuma ili kukondoka zake
Rex: nina ujumbe wako bwana Asim uliotumwa tarehe kumi mwezi wa pili elfu mbili na arobaini na nne kutoka kwa bi aisha malik akaunti namba mia moja na kumi koma makene koma mwezi mweusi
Baada ya kusikia lile jina Asim aligeuka nyuma haraka na kumsogelea yule roboti karibu
Asim: nani? Bi nani?
Rex: samahani nashindwa kuufungua ujumbe kwasababu ya upungufu wa nafasi katika diski
Asim: kwanini huwezi kufungua , fanya kitu basi
Rex: Nitafuta data zisizo hitajika ili kupata nafasi Zaidi kwenye diski, kitendo hiki kitachukua muda kidogo
Asim:Itachukua muda gani?
Rex:Siwezi kujua hilo kwa sasa hivi
Asim: Twende ndani
Alimchukua yule roboti na kwenda nae ndani kwani alikaa nje kwa muda mrefu na ilikuwa hatari sana kwake . Alikaa ndani na yule roboti akisubiria kwa takribani masaa matatu ili yule roboti azifute data alizosema na ampatie ujumbe wake, lakini bado data hazikuweza kufutika na ilimlazimu asubirie Zaidi , na kulikuwa na kimya kirefu mpaka yule roboti alipouliza baada ya kuona picha ya bi aisha ukutani
Rex: Una uhusiano gani na daktari aisha? Kwa sababu alinisisitiza sana kukufikishia huu ujumbe. Je wewe ni mwanae? Alikuwa anakutaja kila siku.
Rex aliuliza maswali ambayo hayakujibiwa hata kwa kifupi lakini aliendelea kuuliza baaa ya kuuona ule mtambo aliokuwa umetupwa chini
Rex: Ulikuwa unatengeneza mashine ya muda ? haikufanikiwa kwa sababu ya nyaya zilizogusana katika kikinzani cha tatu, kama utaweza kurekebisha basi utafanya kazi. Kwani unataka kwenda kwenye mwezi mweusi? Lakini Daktari Aisha alikuwa anataka kurudi huku
Asim: alikuwa anataka kurudi huku? Mbona hajarudi?
Rex:Hakuweza kufanya hivyo , walimuua kabla hajaondoka
Asim:Wamemuua?
Rex: ujumbe umemaliza kupakuliwa na utafunguka hivi punde
Sauti ya mama yake Asim ilisikika baada ya mlio wa bipu ikisema
‘Asim …. Ni miaka mingi tangu niondike na najua unajaribu sana kuja huku .Nina Imani kuwa utabaki salama miaka yote na nina Imani unanipenda …. Nakupenda pia. Huu ni ujumbe wangu wa mwisho kwako , mwezi mweusi sio makao yetu ila ni matokeo ya ubadhilifu wetu. Nilitamani sana kusaidia kupalinda nyumbani ila sikupata nafasi ya kufanya hivyo ila wewe unaweza kufanya hivyo , hatma ya nyumbani kwetu ipo mikononi mwako, Rex atakupatia mbegu, ipande na urudishe uhai nyumbani , na hilo ndo jambo pekee ninalotamani litokee , naamini utalifanikisha hilo, nakupend…..’
Ile sauti ilikata na kwenye kifua cha Rex kulifunguka na kutoka mbegu . Asim aliichukua ile mbegu na kuishika mkononi huku akiwa ameduwaa bila kujua cha kufanya kwa wakati ule.
Asim: nifanye nini……..?

Upvote
0