Nyumbanitu: Msitu wa ajabu mkoani Njombe wenye kuku weusi, ng'ombe weusi, mbuzi weusi na kondoo weusi

Ili kurudisha mvua, waumini wote waliohusika na maombi hayo, waliitwa ili waombe msamaha kwa mizimu kwa kuleta kaniki, kuku mweusi, ng'ombe mweusi na sarafu ambazo waliiba mahali hapo.
Red: sidhani kama kulikuwa na 'ulokole' humo!
===
Njia mbadala yakutoka msituni kwa wanaopotea (Nawaza tu!)
*****
Hao wanaopotea....wanatakiwa wanyooshe njia moja kufuata jua lilipo huku wakiangalia saa! Mfano, kama nia asubuhi wakiamua kutoka kwenye msitu kupitia upande wa mashariki, basi wanalifuata jua linapotokea. Ikifika saa tano wanapumzika....mpaka saa tisa alasiri. Wanaanza safari tena mara hii watembee kutoka msituni wakiwa wamelipa mgongo jua. Ikifika saa kumi na mbili jioni wanapumzika mapaka kesho yake asubuhi ambapo watarudia mtindo wa jana yake. Wasijaribu kutumia mwezi...kutoka msituni unaweza kuwapoteza, maana hauelewi kwani kuna siku upo nusu, muda mwingine ndiyoauonekani kabisa!
 
duh ni hatar bongo kuna maajabu mengi
 
Mkuu wabongo watu wa ajabu sana, wazungu wanakuja kufanya utalii hapa lakini wazawa wapowapo tu!
[emoji28]sisi tunapenda story za vijiweni,haya mambo ya mali za mjerumani yapo miaka na miaka ingetakiwa watu wawe wameshafika hizo sehemu wamepiga na picha
 
Nenda Njombe halafu ufike nyumbanitu ukahakikishe acha porojo!

Inakusaidia nini kusambaza uwongo kwa Wajinga wenzako? Ume photoshop picha, halafu unataka kutuambia huu muujiza ni wewe ti dunia nzima unajua? Pia nyie MODS, ujinga kama huu msiwape watu nafasi wausamabaze.
 
Inakusaidia nini kusambaza uwongo kwa Wajinga wenzako? Ume photoshop picha, halafu unataka kutuambia huu muujiza ni wewe ti dunia nzima unajua? Pia nyie MODS, ujinga kama huu msiwape watu nafasi wausamabaze.
Mkuu wewe sio mzima mimi sijaweka picha ebu angalia vizuri aliyeweka picha ni mtu mwingine!
 
Mh hizi picha umetuibia master....si ulisema kuku midomo rangi nyekundu?afu mbona kama zimepigwa kiphoto shoot kabisa ni kama kuku wanaofugwa?
 
Picha is not really from nyumba nitu ila simulizi yake ni ya kweli...na kuna PhD mmoja wa UDSM anaitwa mpalanzi kaandika kuhusu hayo.
 
Mambo ya kishirikina hayo yatarudisha nyuma maendeleo ya eneo na kuwapeleka watu jahanamu.Lakini ngoja siku moja niingie huko na watu wangu kama watalii.Tuzunguke kwenye vichochoro vyote vya huo msitu na tunasoma dua kimoyomoyo. Hakuna jini atakayetudhuru na tukiondoka wote watahama.Baada ya hapo mtagundua kichaka kimoja kimoja cha huo msitu kinaungua na itakuwa mwisho wa ushirikina.
 
Wamekazana kuroga tu. Ndio maana Njombe inaongoza kwa utapiamlo
 
Hii mbinu hutumika katika misitu yote au huu tu
 
Walokole walishindwa wewe utaweza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…