Nyumbanitu: Msitu wa ajabu mkoani Njombe wenye kuku weusi, ng'ombe weusi, mbuzi weusi na kondoo weusi

Vp kuhusu wataalamu na mabingwa wa uganga na uganguzi,wapo?, km wapi ni sehemu gn ya mkoa wa njombe?
 
3 Aug 2019
Kijiji cha Mlevela, Njombe
Tanzania

Msitu wa Nyumbanitu, Wanging’ombe Njombe Tanzania

Naibu waziri wa utamaduni na michezo Mh. Juliana Shonza afika pahala pa tambiko Nyumbanitu Njombe


Aonana na chifu wa kabila la Wabena aliyeongozana na wazee, kisha Naibu waziri wa habari, utamaduni sanaa na michezo Mh. Juliana Shonza ameombewa baraka ndani ya msitu wa Nyumbanitu wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe Tanzania mara baada ya kutembelea kivutio hicho cha utalii chenye historia kubwa pamoja na sifa ya kupatikana kuku weusi.

HALMASHAURI YA WILAYA YA WANGING’OMBE, NJOMBE TANZANIA

IDARA YA ARDHI NA MALIASILI

VIJUE VIVUTIO VYA UTALII KATIKA WILAYA YA WANGING’OMBE

Wilaya ya Wanging’ombe imebahatika kuwa na vivutio vingi vya utalii ambavyo vinaweza kuchangia

mapato makubwa kutokana na wageni mbalimbali wanaoweza kutembelea vituo kwa ajili ya kujionea

maajabu mbalimbali katika vivutio hivyo. Vivutio vinavyopatikana katika wilaya ya Njombe ni pamoja

na Mapango na Msitu wa hifadhi wa Nyumbanitu, mwamba wenye ramani ya bara la Afrika, pori la

akiba la Mpanga Kipengere, Eneo la ardhi oevu la Lihogosa, Kilele cha mlima wa Fulanyingi, eneo la

kihistoria la Mdandu, Mapango na Msitu wa Mayiviyivi na Kanisa la kilutheri la Kidugala.

A. MAPANGO NA MSITU WA NYUMBANITU

Mapango na Msitu wa Nyumbanitu viko katika kijiji cha Mlevela, kata ya Igima tarafa ya Mdandu.

Msitu huu ni wa maajabu sana kwani miti yake na mimea yake iko pale kwa karne nyingi.

Inaaminika kuwa makabila mengi ya mikoa ya Iringa, Mbeya, Morogoro na Ruvuma yana

asili ya eneo la Nyumbanitu na kuwa wahenga wa wabena walizikwa katika eneo hili.

Sifa za Pekee za Msitu na Mapango

a. Uwepo wa eneo la Tambiko.

b. Kuwepo kwa kuku weusi ndani ya msitu wasiofugwa.

c. mapango makubwa ambayo watu zaidi ya mia moja

wanaweza kuishi kwenye mapango. Mapango hayo

yalikuwa yanatumika sana wakati wa vita.

d. Aina (Sp) pekee za miti.

Aina ya Utalii unaofaa

a. Utalii wa kiutamaduni.

b. Utalii wa kupiga picha.

c. Utalii wa kutembelea na

kupumzika kwenye mapango.

Msitu wa Nyumbanitu Msitu wa Nyumbanitu Mapango ya Nyumbanitu

S. L. P 624

NJOMBE, TANZANIA
Source : Utalii | Wanging'ombe District Council
 
Ulicomment kama umekatwa kichwa njoo na hayo majini ya kiarabu,
Ujaribu huku Nyumbanitu halafu uone utakavyo fanywa hamna,

Germans walisanda na uchawi wao kutoka Bavaria uje uweze wewe mwarabu koko?

Fa masikhara nini?
😁😁
 
Picha za hao kuku ni bosheni. Ume download
 
Chai tu hii
 
Picha umezipata google

 
Hawa kuku ni wa mayai wanatoka malawi......
 
Hawa kuku ni wa mayai wanatoka malawi......
Malawi ipi mkuu? Mbona humo ndani ya msitu hakuna sehemu inaitwa Malawi?
Soma vizuri maelezo ya mtoa mada Ben Zen Tarot halafu urudi hapa kuja kurekebisha ulicho andika kama koment.
 
Malawi ipi mkuu? Mbona humo ndani ya msitu hakuna sehemu inaitwa Malawi?
Soma vizuri maelezo ya mtoa mada Ben Zen Tarot halafu urudi hapa kuja kurekebisha ulicho andika kama koment.
Hao kuku ulioweka hapo ni wa malawi umetoa google....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…