Nyuzi nyingi za kisiasa zina muelekeo wa kinajimu

Nyuzi nyingi za kisiasa zina muelekeo wa kinajimu

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2016
Posts
14,311
Reaction score
36,056
Habari wana JF,

Nimesoma nyuzi nyingi za kisiasa humu ndani lakini maudhui yake ni ya kinajimu zaidi. Mara utasikia chama hichi kitashinda mara kile kitapata wabunge wachache na kadhalika nakadhalika. Tuwaachie wanajimu kazi yao, tusubiri 28 October.

Jiratibu.
 
Kuna msemo kwamba 'nyoka huuma afikiapo' - yaani akifikia kwenye mguu hawezi kuuma kwenye mkono, bega au kichwa. Huwa nina'admire' watu wanao'reason' maana wanakupa changamoto na wewe ujifunze kujenga hoja kama wao. Lakini si hivyo kwa wachangiaji walio wengi. Hayo unayoita 'maudhui ya kinajimu' mimi huyaita 'kupiga ramli'. Kumbe na wewe umeona hivyo. Michango mingi hakuna kujenga hoja, bali ni kupiga 'ramli'.

Hii ina maana wachangiaji wengi wameacha kuwa 'intelligent thinkers' na hali kama hii sijui ni matokeo ya elimu tuliyoipata na kutojiendeleza au ni matokeo ya kuweka elimu pembeni na kuingia kwenye 'ramli' au 'unajimu'?

Ukitaka uhakikishe hili, sema umekutana na misukule kijijini kwako na uone jinsi watu walivyo interested kuelezea inavyofanana na ile waliokwishaiona hata kama umebuni tu hadithi hiyo. Nawasikitikia sana watoto wa watoto wetu. Sijui watajifunza nini kutoka kizazi chetu. Inabidi tubadilike sana.

Si unakumbuka pia yale mashindano ya vyuo vikuu mbalimbali Afrika (kuulizwa maswali ya 'general knowledge') tulivyokuwa tunapigwa mtama? Shame upon us!
 
Kuna msemo kwamba 'nyoka huuma afikiapo' - yaani akifikia kwenye mguu hawezi kuuma kwenye mkono, bega au kichwa. Huwa nina'admire' watu wanao'reason' maana wanakupa changamoto na wewe ujifunze kujenga hoja kama wao. Lakini si hivyo kwa wachangiaji walio wengi. Hayo unayoita 'maudhui ya kinajimu' mimi huyaita 'kupiga ramli'. Kumbe na wewe umeona hivyo. Michango mingi hakuna kujenga hoja, bali ni kupiga 'ramli'. Hii ina maana wachangiaji wengi wameacha kuwa 'intelligent thinkers' na hali kama hii sijui ni matokeo ya elimu tuliyoipata na kutojiendeleza au ni matokeo ya kuweka elimu pembeni na kuingia kwenye 'ramli' au 'unajimu'? Ukitaka uhakikishe hili, sema umekutana na misukule kijijini kwako na uone jinsi watu walivyo interested kuelezea inavyofanana na ile waliokwishaiona hata kama umebuni tu hadithi hiyo. Nawasikitikia sana watoto wa watoto wetu. Sijui watajifunza nini kutoka kizazi chetu. Inabidi tubadilike sana. Si unakumbuka pia yale mashindano ya vyuo vikuu mbalimbali Afrika (kuulizwa maswali ya 'general knowledge') tulivyokuwa tunapigwa mtama? Shame upon us!

Ni kweli kabisa, tunasoma ila hatuelimiki. Wengi tunasema itakua hivi au vile bila kutoa maelezo ni kwasababu gani unaamini hivyo ndivyo itakavyokua. Kimsingi, siasa zinaelekea kuwa kama ushabiki wa simba na yanga, hakuna objectivity.

Ilimradi mimi ni mshabiki wa Yanga basi, simba ata acheze mpira kama Barcelona sikubali. Nafikiri tutoke kwenye huo mtego.

Vyama vya siasa ni vyombo vya kiuongozi vinavyopaswa kuwatumikia wananchi kwa kutengeneza mifumo ya kiuongozi na kiuchumi itakayo boresha maisha ya watu. Hivyo basi, kama hauvutiwi na mfumo mmoja unachagua mwingine, si kesi wala dhambi.
 
Back
Top Bottom