Kuna msemo kwamba 'nyoka huuma afikiapo' - yaani akifikia kwenye mguu hawezi kuuma kwenye mkono, bega au kichwa. Huwa nina'admire' watu wanao'reason' maana wanakupa changamoto na wewe ujifunze kujenga hoja kama wao. Lakini si hivyo kwa wachangiaji walio wengi. Hayo unayoita 'maudhui ya kinajimu' mimi huyaita 'kupiga ramli'. Kumbe na wewe umeona hivyo. Michango mingi hakuna kujenga hoja, bali ni kupiga 'ramli'. Hii ina maana wachangiaji wengi wameacha kuwa 'intelligent thinkers' na hali kama hii sijui ni matokeo ya elimu tuliyoipata na kutojiendeleza au ni matokeo ya kuweka elimu pembeni na kuingia kwenye 'ramli' au 'unajimu'? Ukitaka uhakikishe hili, sema umekutana na misukule kijijini kwako na uone jinsi watu walivyo interested kuelezea inavyofanana na ile waliokwishaiona hata kama umebuni tu hadithi hiyo. Nawasikitikia sana watoto wa watoto wetu. Sijui watajifunza nini kutoka kizazi chetu. Inabidi tubadilike sana. Si unakumbuka pia yale mashindano ya vyuo vikuu mbalimbali Afrika (kuulizwa maswali ya 'general knowledge') tulivyokuwa tunapigwa mtama? Shame upon us!