Nyuzi zimekuwa nyingi humu kama vile watu hawataki kujifunza

changaule

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2020
Posts
6,039
Reaction score
10,151
Naona zimeanzishwa nyuzi nyingi humu za utabiri wa Raja kumshushia Simba kipigo, binafsi pamoja na ushabiki wangu wa Yanga lakini inapofikia mechi ya kimataifa uwanja wa Mkapa kwa timu ya Simba huwa naiheshimu mno. Hata wawe na timu ya ovyo kiasii gani lakini utaona hao wachezaji wanavyobadilishwa kuwa akina Mbape. Yaani tunaongalia tunawaona akina Bocce na Chama lakini kumbe sio wao ni wakina Halland ndio wanaocheza.

Watu wanaisifia Raja Casablanca kuwa ni timu bora hilo mimi silipingi ni sahihi kabisa je lakini ni bora kuliko Al Ahly? Maana Al Ahly hakuwahi kuambulia hata sare kwenye uwanja wa Mkapa dhidi ya Simba. Simba wamekuwa wazuri wa kutumia silaha zao za vita unapomfata kwake, hata uwe umeendelea kiasi gani kwa kuwa na mabomu ya nyuklia lakini hizo hizo rungu, panga na sime zitafanya kazi ya kummaliza mpinzani kwa mbinu wanazojua wao. Hivyo mashabiki wenzangu wa Yanga tujifunze tu kukubaliana na hali, Raja kutoka sare au kuifunga Simba itakuwa tu kama surprise ila sio kwa history ya Simba kwenye huo uwanja.

Kingine kuhusu ahadi zilizotolewa na wana siasa akiwemo Raisi wa J.M.T hizi ahadi wameshindwa tu kusema waliolengwa ni nani, imewekwa in general ili tu kubalansi mzai. Ila kama mzazi unajua tu kuwa nina watoto wawili, mmoja ni kichwa na mwingine ni kilaza. Huyu kichwa hata asipotangaziwa ahadi lakini anajiweza mitihani mingi mikubwa mikubwa anafaulu lakini huyu kilaza anaishia tu madarasa ya awali. Hivyo anayebustiwa hapa ni huyu kilaza ili naye asiwe mnyonge wa kufeli feli kila miaka.
 
Endeleeni kuishi kwa kukariri. Football haipo hivyo na kamwe haijawahi kuwa hivyo, eti kisa Al Ahly alikufa kwa Mkapa basi na Raja atakufa kwa Mkapa.

Siku zote timu Bora ndio yenye nafasi kubwa ya kushinda mchezo, kinyume na hapo huwa ni Bahati tu na kumbuka bahati hutokea mara chache sana.
 
Kisa timu fulan huwa inafungwa hii itafungwa
Pua pua pua
 
Kajiandaeni na timu yenu kesho kuna ndombolo ya solo uwanjani...bendi za kikongo zitatumbuiza uwanjani...
 
Ngoja tusubiri tuone. Dakika 90 zitatoa matokeo sahihi. Wa kucheka atacheka, na wa kulia atalia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…