Nyuzimtandao muhimu kwa Majarida ya Kisomi (Academic Journals) na Hesabu

Nyuzimtandao muhimu kwa Majarida ya Kisomi (Academic Journals) na Hesabu

Rugemeleza

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2009
Posts
668
Reaction score
136
Napenda kuwatumia nyuzimtandao hizi ambazo zitawezesha vyuo vyetu na wasomi huko nyumbani Tanzania kuweza kupata na kushusha/pakua makala mbalimbali za kisomi yasiyopungua 8,000. HINARI, AGORA, OARE and ARDI Research4Life - About us.

Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zimesamehewa kulipia ada za uanachama wa majarida hayo. Sharti ni kuwa vyuo vyetu vijiunge na kujisajili kuwa na haki ya kupata majarida hayo. Vyuo vijisajili na kuwawezesha walimu na wanafunzi wao kuweza kuyapata majarida yao. Nilituma kwa watu wachache huko nyumbani lakini sina uhakika kama habari hii imewafikia watu wengi na ndio maana nikaona niiweke hapa. Waratibu wa Mtungo(Blog) hii naomba muipe habari hii uzito wake.

Uzimtandao wa pili ni huu wa Khan Academy ambao ni mtandao wenye uvumbuzi wa hali ya juu wa namna ya kufundisha hesabu. Lengo ni kuhakisha kuwa mwanafunzi anajifunza kwa uangalifu hesabu na kupitia hatua zote za kila somo. Pale tu anapoweza kuyajibu maswali ya somo husika kwa usahihi ndipo anaweza kufungua na kujifunza somo linalofuata. Ninawaomba ndugu zangu muisambaze kila shule nchini kwetu. Tunajua umuhimu wa kuelewa hesabu lakini shule zetu nyingi hazina walimu wazuri wa hesabu. Ninaelewa kuwa shule nyingi kama asilimia pengine 90 hazina huduma ya mtandao lakini tuanze na zile zenye nazo. Tuelimishane ndugu zangu.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Back
Top Bottom