Si mtaalam sana ila nitakuelekeza kadri nijuavyo na mengine utatafuta.
1.Usafi wa nywele zako
Osha nywele zako kila baada ya wiki 1 na shampoo zitakate na suuza kwa maji mengi.
2. Baada ya kuosha na kuzikausha unapaka conditioner unayopenda iwe ya dukani au ya asili, unajifunika kwa mfuko wa plastiki au kofia ya plastiki unakaa nayo kichwani kwa muda wa lisaa 1 au na zaidi yaani ww tu, baada ya hapo unasafisha conditioner yako kwa maji mengi si lazima uoshe tena shampoo
3. Baada ya kuzikausha unapaka mafuta yako unayopenda ila nakushauri tumia mafuta ya maji ni mazuri,
mimi natumia mafuta ya nazi yanaitwa parachute na castor oil nimepunguza kidogo kidogo nimeyachanganya kwenye chupa nyingine. Ndio napaka mchanganyiko huo kwenye ngozi hadi juu ya nywele zangu
4. Baada ya hapo unapaka hair cream/ leave conditioner yako juu juu ya nywele isifike kwenye ngozi
5. Halafu unaweza kusuka mtindo ambao utalinda nywele zako zisikatike kama mabutu, twist, Mnyoosho/ twende kilioni hata kama ukiinganisha na rasta lakini mtindo ambao haukati nywele.
6. Na kuzinyunyuzi maji kila asubuhi kabla ya kuendelea na shughuli zako ile zisikae kavu na kabla ya kulala vaa kofia ya satin au funga kitambaa cha satini.
Ukifanya hivyo na kufuata ratiba uliyojiwekea zitakua vizuri tu.