Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Kuna mambo ya kushangaza ambayo kwasababu ileile ya kimapokeo na mazoea huwa hatuyahoji au hatuna muda wa kufuatilia na pengine tunaridhika tu na hivyo yalivyo.
Nywele hizi zetu za kichwani zinabeba siri kubwa ambayo ina mawasiliano ya moja kwa moja na kuzimu au na roho zinazotangatanga.
Hebu tujihoji haya;
- Kwanini baadhi ya imani ni marufuku na hairuhusiwi kwa mwanamke kuonyesha nywele zake hadharani?
- Kwanini mchawi/mwanga anapokamatwa hukatwa nywele zote ili kummaliza nguvu zake?
- Kwanini chizi kichaa au mwendawazimu hunyolewa nywele kama sehemu ya tiba?
- Kwanini wachawi na waganga wengi hutumia nywele kama sehemu ya uchawi/ulozi wao?
Historia ya nywele kuhusiana na roho na nguvu za kiza inaanzia mbali sana miaka elfu nyingi iliyopita kwenye habari za Biblia takatifu kisa cha Samsoni na Delilah pale Mwenyezi Mungu alipoweka nguvu isiyomithilika kwenye nywele za Samsoni lakini shetani kupitia Delilah alimrubuni Samsoni na Samsoni akatoa siri ya nguvu zake.
Ni kutoka hapo ile nguvu ya kimungu iliyowekwa kwenye nywele za Samsoni iligeuka na kuwa nguvu ya kishetani na kufanya maangamizi makubwa, tangu hapo nywele imekuwa ni kitu kinachohusishwa na roho chafu na mapepo.