Nzi,Mbwa,Mbu... Kwanini si Nnzi,Mmbwa,Mmbu n.k?

Nzi,Mbwa,Mbu... Kwanini si Nnzi,Mmbwa,Mmbu n.k?

Kutoka Mirembe

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2014
Posts
294
Reaction score
87
Hodi hodi wataalamu wa Lugha.
Kuna maneno kama nzi[linasomeka nnzi]
mbwa[mmbwa] na mbu[mmbu].
Ilikuwaje maneno hayo yakaandikwa tofauti ya matamshi yake?
Wadau naombeni msaada huyu mdudu anaitwa "Inzi" au "Nzi"... Kama unareferenc ni vizur zaidiView attachment 150875
Tunaandika lugha yetu kwa kutumia maandishi ya watu, huwezi kuandika Kiswahili, Kibarbaig, Ki Hottentont, Kichina au Ki-Bushman kwa kutumia alphabet ya Kirumi.

Tunahitaji herufi zetu.

The closest approximation is a reverse silence letter, Kiswahili hakina doubling letters, kwa hiyo, kwa kuibia hii alphabet ya Kirumi, maandishi yanaandikwa "mbu" "nje" "mbwa"

Compromise ilitakiwa iwe "m'bu" "n'je" "m'bwa" lakini kamwe si "mmbwa".
 
Historia inaonesha kuwa lugha ya Kiswahili iliwekwa kimaandishi kwa mara ya kwanza na wazungu ambao hawakuweza kuandika maneno ya Kiswahili kama yalivyotamkwa na Waswahili, ila waliandika kama walivyotamka wao.
Ukitazama hata majina ya Mikoa walibadilisha kulingana na matamshi yao mf. Idodomya ikawa Dodoma (ingawa hili sio jina la kiswahili ni mfano tu wa namna wazungu walivyo badili baadhi ya mambo)
 
Herufi mbili kwa pamoja kwenye Kiswahili huunda silabi, mfano b+a=ba, ila kuna herufi ambazo zinaweza kusimama zenyewe bila kuambatana na herufi nyingine kuunda silabi, herufi "m" na "n" ni herufi hizo na kwenye matamshi yake huwa zinatiwa mkazo, mfano m'bwa, n'zi, hayo maneno kila moja lina silabi mbili na si moja.

Sasa kwenye kiingereza hakuna maneno ambayo huanza na mtiririko wa matamshi kama hayo uliyotaja, sasa wanachofanya ni kuongeza irabu mwanzoni ili imsaidie kutamka (phonotactic constraints). Ndio wanasema 'inzi', lugha nyingine za hapa Tz wanapata tabu pia ndio maana husema "umbu" badala ya "mbu". Hizi huwa ni athari ya lugha mama (mother tongue).
 
MANENO kama nje, mbu, nzi ni athari za wageni katika kipindi cha kukua Na kuenea kwa kiswahili ktk shughuli za utawala walikuwa wajerumani ukisoma historia ya kiswahil
 
Neno lolote la kiswahili lenye silabi moja na ilabu moja hupelekea kurudiwa herufi ya kwanza katika matamshi
 
kimsingi katika lugha ya kiswahili kuna baadhi ya sauti huweza kuaaikika katika matamshi lakin sauti hizo hudondoshwa katika maandishi kwasababu za msingi. sababu mojawapo ni kwamba katika lugha ya kiswahili NADHARI mbili zinapofuatana na kisha kufuatiwa na KONSONATI basi NADHALI moja lazima idondoshwe katika maandishi ( Nnaposema NADHARI Namaanisha sauti M,N na NG')
 
kimsingi katika lugha ya kiswahili kuna baadhi ya sauti huweza kutumika katika matamshi lakin sauti hizo hudondoshwa katika maandishi kwasababu za msingi. sababu mojawapo ni kwamba katika lugha ya kiswahili NADHARI mbili zinapofuatana na kisha kufuatiwa na KONSONATI basi NADHALI moja lazima idondoshwe katika maandishi ( Nnaposema NADHARI Namaanisha sauti M,N na NG')
 
naunga hoja
 
Neno lolote la kiswahili lenye silabi moja na ilabu moja hupelekea kurudiwa herufi ya kwanza katika matamshi

Kweli?

Hebu twende kwenye kutamka "mbu" ukitofautisha na "mbwa"

Nini kilifanya neno "mbumbumbu" litamkwe kama lilivyo bila kukazia "m" ilhali ukitaka kusoma neno la mdudu "mbu" yakupasa ukazie herufi "m"?. Hii pia ni kama pia ukitamka neno nzima hukazii n kama ukitaka kusoma neno la mdudu "nzi"
 
kimsingi katika lugha ya kiswahili kuna baadhi ya sauti huweza kutumika katika matamshi lakin sauti hizo hudondoshwa katika maandishi kwasababu za msingi. sababu mojawapo ni kwamba katika lugha ya kiswahili NADHARI mbili zinapofuatana na kisha kufuatiwa na KONSONATI basi NADHALI moja lazima idondoshwe katika maandishi ( Nnaposema NADHARI Namaanisha sauti M,N na NG')

Sawa hebu tuambie kwa mfano ikawaje mdudu "mbung'o" akatamkwa bila kukazia herufi "m" lakini kiongozi wa kisıasa "mbunge" neno likakaziwa herufi m?

vipi kuhuşu tofauti ya matamshi kwa kuusoma mkoa wa "Mbeya" na tabia ya umbea au mtu "mbea".

Msaada hapo tafadhali. Ohoo kumbe hata neno tunakazia herufi "m"!!!!!

kama hutajali Kiranga naomba pia uelewa wako hapa. Nimekusoma hapo juu ushawishi wako lakini naona bado kuna utata kwa badhi ya maneno yanayofanana lakini hutofautiana kutamkwa kulingana na sentensi inataka kuzungumzia kitu gani.

Wa nyumbani Kaizer najua sekondari ulipata A ya Kiswahili. njoo hapa tafadhali.
 
Last edited by a moderator:
ingawa natambua kuna tofaut mda mwingne kati ya uandishi na utamkaji wa maneno maneno mfano huku kwetu kuna sehem inaitwa mbande lakin inatamkwa m~bande tofaut na mbagala ambayo hutamkwa mbagala
 
Back
Top Bottom