Nzige Wavamia Kilimanjaro

Nzige Wavamia Kilimanjaro

chiwanga11

Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
72
Reaction score
107
Mkoa wa Kilimanjaro eneo la Siha, Nzige wa Jangwani wamevamia. Si mchezo ni wengi balaa.

-----+

Kundi la Nzige waharibifu wa jangwani limeingia wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro Kaskazini mwa Tanzania na kuibua hofu ya uharibifu wa mazao ya chakula.

Wilaya hiyo inazalisha mazao mbali mbali ya chakula na kibiashara kama mahindi, mboga, maharage na mengineyo.

Sio mara ya kwanza kwa uvamizi wa kuripotiwa katika wilaya ya Siha, siku za hizi karibuni.

Taarifa hizi zinakuja wakati ambapo kikosi cha wataalamu kinaendelea na kazi ya kuwanyunyizia dawa wakitumia ndege mkoani Arusha kwenye wilaya za Longido na Simanjiro ambapo waliripotiwa mwishoni mwajuma.

Tayari Waziri wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda na jopo la wataalamu wameshafika mkoani Kilimanjaro kutathimini athari na kuweka mikakati ya kuwaangamiza wadudu hao ambao huzalia kwa wingi na kwa muda mfupi.

Wilaya zilizoshambuliwa awali hazikuwa na hofu kubwa ya uharibifi wa mazao kwani makundi hayo yalishambulia zaidi maeneo ya malisho ya mifugo.

Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, amesema kazi ya kuwadhibiti bado inaendelea kwani wadudu hao waharibifu walivamia maeneo ya malisho na tayari asilimia kubwa ya eneo hilo limeshapuliziwa dawa ambayo kwa mujibu wa wataalamu matokeo yake huanza kuonekana ndani ya saaa 24 hadi 72.

Wananchi wameendelea kuonywa kuwa waangalifu kutokula au kuokota nzige hao au kulisha mifugo kwenye maeneo yaliyopuliziwa dawa, huku shule zikiendelea kufungwa kupisha zoezi hilo.

Chanzo: BBC

========


 
Mkoa wa Kilimanjaro eneo la Siha, Nzige wa Jangwani wamevamia. Si mchezo ni wengi balaa
Wametokea arusha mkuu, walianza kuvamia Longido, Arusha naona wamevuka border, nilisikia serikali imepanga kupeleka ndege ya kunyunyiza dawa, habari hii niliisikia tangu juzi kama siku tatu au nne zimeshapita!
 
Kuna haja ya kupambana nao maana wataleta hali ambayo sio nzuri huko mbeleni.
 
Wakija wazalendo watasema huna mamlaka ya kutoa hiyo taatifa, hayo ni maoni yako !
 
Back
Top Bottom