Exaud J. Makyao
JF-Expert Member
- Nov 30, 2008
- 1,518
- 24
Tunajifunza kwamba Rais wa nchi za Afrika "hakosei" kuchagua baraza la mawaziri. Akimteua fisadi (bwana asifiwe), akimteua mshikaji (haleluya), akimteua kihiyo (amina).
Rais wa Marekani Barack Obama amekubali kwamba alifanya kosa kuhusu uteuzi wa baraza lake la mawaziri .
Wawili kati ya wanasiasa aliowateua kutoka chama chake cha Democratic, walitiliwa mashaka kuhusu uaminifu wao binafsi katika ulipaji kodi.
Hatimaye Wanasiasa hao wawili; Seneta Tom na Bibi Nancy, waliamua kukataa kupokea nyadhifa walizopewa kutokana na tuhuma za kutokuwa waaminifu katika ulipaji kodi zinazowahusu wao binafsi.
Tunajifunza nini kwa nchi zetu za Afrika?
Kwa Obama ni muungwana.Kwa Pinda mnyamwezi.Mwanakijiji upoo?Inatufundisha kuwa Muungwana anapokosea.... na ikijulikana kuwa amekosea basi apaswa kujirudi na kuomba radhi... na kama kuna maamuzi mazito aliyoyafanya kimakosa basi na ayatengue. Huo ndio uongozi uliopevuka. Sio huu wa Kikwete na Sisiem... Chenge amekumbwa na kashfa ya Mabilioni ya Radar... huyo huyo anapewa kamati ndani ya Sisiem kuchunguza uhalali wa ukodishwaji wa jengo la UVCCM. Halafu yanatokea magazeti yanaandika... chenge aula tena sisiem... wizi mtupu!!!!!