Kwani Biblia inatajwa kwenye Katiba kama kitu cha lazima kwenye kiapo Marekani? Sidhani. Kutumia Biblia ni chaguo la anayeapa (kama ilivyo Tanzania)
Iwapo kiapo cha kwanza kilikuwa valid, basi mara ya pili Obama "alirudia" kiapo. Kurudia kiapo ni kuapa mara mbili? Kwa mfano, wengi tunapenda kurudia ahadi za ndoa tunaposherekea Jubilee ya Ndoa (25 years). Kwa kurudia huko, utasema tumeoa mara mbili?
Kama kiapo cha kwanza cha Obama hakikuwa valid, basi aliapa alipofanya hivyo mara ya pili. In either case aliapa, validly, mara moja tu.