Obama anaweza kuunda tume ya kupitia Katiba ya Marekani?

Obama anaweza kuunda tume ya kupitia Katiba ya Marekani?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Hivi Rais Obama anaweza akaamka na kuamua siku moja kuunda Tume ya Kupitia Katiba Mpya na kuwaahidi wananchi wa Marekani ambao baadhi yao wanaona Katiba inahitaji mabadiliko Katiba Mpya kwa ajili ya miaka mingi ijayo. Nini kitatokea endapo atafanya hivyo?
 
Haiwezekani asilani, kwani Rais Obama ana mwanasheria mkuu makini na asiyekuwa mwoga wa kusema kweli. Zaidi ya hilo ana waziri wa sheria aliyemakini.
 
JK anataka kuikumbatia mchakato ili waweke wanachoamini kuwa kitawalinda.....inabidi mchakato uende bungeni
 
Kikwete decision very undemocratic,why he is trying is to steal our game
 
Hivi mimi nashangaa, kila atalofanya JMK ni baya. "Damned if you do damned if you don't", kwa nini? Au ndio...?
 
CCM, hapana / Democrats watampiga chini mara moja maana hafanyi kazi kwa kufuata sera zake binafsi bali ni kwa kuitegemea na kuitegemeza chama chake kilichompa ufadhili kwa nafasi alionayo.

MAFISADI wachache mlioko ndani ya CCM, mbinu yenu hii imeshaanguka CHALI hata kabla haijaanza kutekelezwa 'and YOU CAN QUOTE ME ON THAT'.
 
Hivi mimi nashangaa, kila atalofanya JMK ni baya. "Damned if you do damned if you don't", kwa nini? Au ndio...?

Jibu ni kwamba UKICHINJA KUNGURU MMOJA basi kutwa kuchwa wako na wewe popote uendako na lolote ulitendalo utajihisi UNADAMU YA KUNGURU tu.

Yote haya ni gharama ya UCHAKACHUAJI na kukosa uaminifu kwa watu unaowatawala.
 
Hivi Rais Obama anaweza akaamka na kuamua siku moja kuunda Tume ya Kupitia Katiba Mpya na kuwaahidi wananchi wa Marekani ambao baadhi yao wanaona Katiba inahitaji mabadiliko Katiba Mpya kwa ajili ya miaka mingi ijayo. Nini kitatokea endapo atafanya hivyo?

Hizi si ndio pumba zenyewe? Kwenda kuifananisha Merekani na Tanzania, mrudishe Obama miaka 50 baada ya US kupata Uhuru halafu tuone hata kama swali lako litawezekana kuulizika. Halafu watu kama wewe mnajiita "great thinkers"? To me, you are just a tinker!
 
Nadhani MMM anauliza juu ya Obama na si JK.Tehe teheee...

Kwanza aulize ni miaka mingapi leo ya Uhuru wa Merekani na wetu? Halafu ajiulize katika miaka ya 50 ya Uhuru wa Merekani angeweza kuuliza swali kama hili? Kama si pumba hizi ni nini?
 
Back
Top Bottom