Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama, anajiandaa kufanya kampeni kwa ajili ya Makamu wa Rais Kamala Harris katika juhudi za mwisho kuelekea uchaguzi.
Obama, ambaye ni Kiongozi mashuhuri wa Chama cha Democratic, ataanza kampeni zake kwa Harris Alhamisi ijayo huko Pittsburgh, huku akipanga kuzunguka majimbo mengi yenye ushindani mkubwa kabla ya Siku ya Uchaguzi, ambayo ni takriban siku 27 kabla ya uchaguzi.
Katika Mkutano wa Taifa wa Chama cha Democratic uliofanyika awali, Obama alimpongeza Harris kwa urithi wake wa kisiasa, akimuelezea kama mrithi wa harakati zake.
Aidha, Obama alielezea jinsi Harris, ambaye ni mwenye asili ya kutoka Jamaica na India, anaendeleza urithi wa harakati zake za kisiasa pia Obama katika mkutano huo alisema, Harris kama Rais, hatazingatia matatizo yake binafsi bali atazingatia matatizo ya wananchi wote wa Marekani.
Kampeni ya Harris imejikita kwenye mabadiliko makubwa baada ya Rais Biden kujiondoa, huku ikiongeza washauri kadhaa wa zamani wa Obama kwenye timu yake na hatua hii inaonesha uhusiano thabiti wa kisiasa na kimkakati kati ya wawili hao.
Soma Pia: Maafisa usalama zaidi ya 700 wamuunga mkono Kamala Harris dhidi ya Trump kwenye Uchaguzi mkuu Marekani 2024
Kwa msaada wa Obama, Harris anatarajiwa kuimarisha nafasi yake katika maeneo yenye ushindani mkubwa, akitafuta uungwaji mkono wa wapiga kura wa makundi mbalimbali