Mjukuu wa kigogo
JF-Expert Member
- Sep 19, 2023
- 445
- 1,094
Kwanza nikupongeze sana OC-CID wilaya ya Bunda kwa ulivyopambana na uhalifu na pongezi zaidi kuuzima uhalifu wa kutumia pikipiki ulioanza kuchukua nafasi hivi karibuni nyakati za usiku. Kiukweli katika historia ya viongozi wachapakazi wa jeshi la polisi wilaya ya Bunda utakumbukwa.
Sasa nataka nikusanue kidogo kuna chimbo wanalokusanyana wahalifu nyakati za usiku na wakati fulani mida ya mchana. Ukiwa maeneo ya Wilson bakery mbele yake kuna gofu moja ambalo linasimamiwa na kijana mmoja aitwaye Makoba. Hapa ndipo vikundi vya uhalifu hukutana nyakati za usiku ambako hupanga mikakati yao mara kwa mara.
Hapa ndio kiini cha uhalifu Bunda kilipo wakabaji wote wa usiku hukutana hapa, wauzaji dhahabu feki hukutana hapa, wabomoaji hukutana hapa yaani mpaka biashara ya pombe haramu na bangi hapa ni makutano.
Kulipata hii eneo ni rahisi tu unaulizia kwa Makoba. Kundi kubwa hapa la wahalifu ni under 18. Hawa ndio tatizo maeneo ya uswahilini.
Kama itakupendeza mkuu anza operation wiki hii
UPDATE:
Hongereni polisi kufika tarehe 1.8.2024 majira ya mchana kwenye hili jengo japo bahati mbaya wahusika walikimbia.Na kukimbia kwao ilikuwa ni baada ya kuliona gari la polisi maeneo husika.Bado nasisitiza hapa ni mahali ambako si salama kabisa. Vijana wahalifu hukutana na kugawana mali walizoiba kama fedha taslimu,simu nk.Lakini pia ni eneo ambalo mikakati ya uhalifu hupangwa.Ni njia ya uchochoro ambapo mabinti wanapopita hupata pia mashambulio ya aibu,kuporwa simu nk kutukanwa nk Mkuu tuma maaskari waadilifu eneo husika.Hili ilishakuwa siyo eneo salama wa wakazi na wapita njia kwa ujumla.