DOKEZO OCD Bunda fanya uchunguzi wa kina juu ya mgambo wako, wanashirikiana na vibaka

DOKEZO OCD Bunda fanya uchunguzi wa kina juu ya mgambo wako, wanashirikiana na vibaka

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Mjukuu wa kigogo

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2023
Posts
445
Reaction score
1,094
Utaratibu wa polisi kutumia Jeshi la akiba almaarufu mgambo katika kukabiliana na matukio ya uhalifu ni suala linahotaji kuungwa mkono na kila raia anayelitakia mema Taifa lake. Na hili halikwepeki popote Duniani.

Kimantiki idadi ya askari ni ndogo na hivyo ulazima wa kuwatumia mgambo haukwepeki. Bahati mbaya zaidi kwa wilaya ya Bunda mgambo wapo kimasilahi zaidi na siyo kupambana na matukio ya uhalifu. Hata operation nyingi za polisi kufanya doria kukamata wahalifu zimekuwa na changamoto mojawapo ni taarifa kuwafikia wahalifu mapema kabla ya utekelezaji.

Lakini pia kuna doria zisizo rasmi ambazo hufanywa na mgambo ili kupata chochote na siyo kupambana na uhalifu. Mfano imekuwa ikitokea mara nyingi mgambo kupita maeneo yaliyokithiri Kwa michezo ya kamari ambapo mwenye chochote kitu hutoa na kuachiwa hapohapo na yule pangu pakavu hupelekwa kituoni. Hapa kweli utegemee kumaliza uhalifu? Siyo rahisi.

Kuna utapeli unaofanywa na vijana wadogo wanaouza dhahabu feki. Hapa lengo siyo kuielezea namna biashara inavyofanyika ila hii biashara Ina back up kubwa sana ya mgambo na baadhi ya askari wasio na maadili. Popote palipo na vijana hawa maarufu kama wauza "Zara" huwa kunakuwepo kundi la mgambo ambao hufuatilia mgao wao kwa mfumo wa (MBWA)-Management by walking Around. Vijana wakishauza "dhahabu" zao mgambo hupata gawio lake na maisha yanaendelea. Huu ni mfano tu katika mengi yaliyo nyuma ya pazia yanayifanywa na mgambo.

Wiki kadhaa zilizopita nilikuwa kwenye pub moja maarufu yenye jina la msanii mmoja maarufu hapa nchini. Akawa ameingia mgambo mmoja ambaye nilimtambua kwa jina la John akiwa anamtafuta mhalifu mmoja. Bahati nzuri alifanikiwa kumkamata ambapo mgambo yule alitumia muda mwingi kumlaumu kijana yule kupata pesa za mauzo kisha yeye (kijana) na wenzake kushindwa kutoa mgao kwa wakati Kwa mgambo na askari fulani ambaye nae yupo kwenye huo mlolongo. Muafaka ulipatikana kwa kijana yule kutoa 10000 na kuachiwa huru. Hii ni hatari sana!

Lakini hilo la wauza dhahabu lilipofikia mgambo huwa wanasafiri na vijana hao kwenda minadani na magulioni. Mgambo hao wakiwa minadani huwa wanavaa "koti" la walinzi wa usalama ila kiuhalisia hufuata mgao kwa vijana husika. Na ukweli ulio wazi vijana hawa hawaogopi chochote na hasa wanapokuwa na pesa mfukoni.

Ushauri sasa;
Kwanza mgambo wafuatao wafuatiliwe nyendo zao kujiridhisha kama bado wana sifa
1. Samwel
2. Hassan
3. John
4. Hassan
5. Chacha
6.Salum
Hawa mgambo wakiendelea kuwepo ni ngumu sana kwa vita ya uhalifu kuisha katika mji wa bunda lakini pia Mkuu wa jeshi polisi ukihitaji kujiridhisha kamata baadhi ya vibaka ongea nao friendly wakueleze namna wanavyotoa mgao kwa wahusika.

NB: Mgambo namba 3 ambaye kapewa mamlaka ya kutembea na pingu pia anaitumia kujinufaisha yeye mwenyewe na siyo kwa maslahi ya nchi.

Majibu ya Jeshi la Polisi ~ RPC Mara: Kama kuna Mgambo wanaodai wanafanya kazi ya Polisi hao ni Wahalifu tu
 
Ishia Kwa mgambo boss! Ukiwaanika polisi ujue wenzako wslioko upelemkuu na tcra na tc watakutambua Kisha watakushughulikia.

Mtoa taarifa hugeuzwa mhalifu.
 
Back
Top Bottom