Wakati wajumbe wakianza kuingia mjini Gairo kwa ajili ya kupiga kura ya maoni kwa waliojaza na kurudisha fomu, mbunge aliyemaliza muda wake Mhe. Shabiby anakabiliwa na wagombea wengine zaidi ya 20. Juzi baada ya kikao cha wagombea wake, amesambaza pesa kupitia kwa wagombea udiwani waliomaliza muda wake wanaoomba tena muhula huu wa pili.
Jana tarehe 18/07/2020 mpambe wàke akiwa na askari walikuwa wakiita wajumbe ili kugawa pesa. Amelazimika kushirikiana na polisi ili kukwepa madiwani hao kukamatwa na polisi. Pili, ni uhakika wa wagawa pesa hao kufikisha pesa kwa wapiga kura. Shabiby ambaye ana mahusiano mabaya na watumishi wa Gairo hasa DC wa hapa amekuwa akikodi wahuni kumtukana DC Huyo na kisha kutoroka.
Mmoja wa wahuni hao ni kaka yake ajulikanae kwa jina la Salehe ambaye kwa sasa ametoroka na kila akitaka kukamatwa OCD amekuwa akimsaidia kutoroka. Katika kikao cha juzi cha wagombea wrote mmoja wa wagombe niliyepata jina moja tu la Omary alilazimika kutolewa nje ya kikao baada ya kumtuhumu mwenyekiti ya wilaya hiyo wa CCM kuwa amekuwa akimpendelea na kumfanyia Shabiby kampeni kama sehemu ya kulipa fadhila baada ya kununuliwa gari aina ya Verossa na mfanyabiashara huyu maarufu wa mabasi, vituo vya mafuta na nyumba za kisasa za kulala wageni.