Katika Hali isiyokuwa ya kawaida, Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Dodoma Mjini na Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya Jumapili tarehe 1 September 2024 walimbatana na wananchi waliovamia Kanisa la AGGCI Kizota kinyume cha Sheria wakati Ibada ikiendelea na kufunga Kanisa Hilo ambalo kwa sasa lipo chini ya mjane ambaye ni Mke wa muasisi wa Kanisa Hilo Marehemu Mchungaji Samson Chipanjilo.
Alipoulizwa na waumini wa AGGCI kutoa barua au maandishi yanayoeleza sababu za kulifunga Kanisa Hilo OCCID alikataa kutoa maelezo yoyote na badale yake alimuagiza mwananchi mmoja kuweka kufuli kwenye kanisa la mjane huyo.
Your browser is not able to display this video.
Your browser is not able to display this video.
Baada ya kufunga Kanisa Hilo, inadaiwa kuwa OCCID aliambatana na wananchi hao na kwenda nao eneo la Chinangali Park na kujipongeza kwa vinywaji kwa kukamilisha jambo hilo, aidha taarifa za ndani zinadai kuwa Kuna kigogo mmoja ambaye anamtumia OCCID na OCD na amewapa Hela Ili wamsaidie kigogo huyo kumpora mjane huyo Hilo eneo kinyume na sheria.
Kuna kanisa hapo Dodoma ni la kilokole miaka kadhaa huko nyuma liliwahi kukumbwa na mgogoro wa umiliki kati ya Mchungaji na Kondoo.
Kondoo walidai kuwa walichanga fedha na kununua eneo na baadae ujenzi.
Baadae wakagundua kuwa hati ya eneo hilo linasomeka jina la Mchungaji na siyo jina la taasisi yaani kanisa. Sikumbuki ni kanisa gani lkn nadhani hii ilitokea 2019 kama siyo 2020.
Huenda likawa ni hili na baada ya mchungaji kwenda Jerusalem kama alivyo ahidiwa basi jamaa wameliamsha tena.