real G
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 5,227
- 5,299
Upekuzi wa hivi punde umebaini kuwa aliyekuwa kiongozi wa mashtaka katika mahakama ya kimataifa (ICC) Luis Moreno Ocampo alifanya kila juhudi kuchelewesha maamuzi kuhusu mashtaka yaliyomkabili Rais Uhuru Kenyatta, naibu wake William Ruto na washukiwa wengine wanne ili kujiondolea fedheha kutokana na uchunguzi duni aliofanya. Upekuzi huo uliofanywa na muungano wa mashirika ya habari nchini ufaransa - Mediapart, umebaini kuwa Ocampo alimshawishi kiongozi wa sasa wa mashtaka ya umma Fatou Bensouda kutamatisha kesi ya Kenyatta, ili kujiondolea mzigo, na kujaribu kuikinga sura ya mahakama.