Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Ruvuma ndugu Oddo Mwisho amesema Serikali inatekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi hivyo ni wajibu wa viongozi kushirikiana na chama ili kuhakikisha kuwa ilani ya CCM inatekelezwa.
Oddo Mwisho amesema hayo wakati akizungumza na viongozi wa Serikali za mitaa wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru ambapo amesema hata kama mtaa au kijiji unaongozwa na mwenyekiti au diwani wa chama cha upinzani ni lazima ashirikiane na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi katika kutekeleza miradi iliyopo katika maeneo yao.