Odinga kwa kuapa kama "Raisi Wa Watu", kavunja sheria gani?

Criterion

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2008
Posts
11,797
Reaction score
11,891
Nimetafakari nikaona niweke huu uzi hapa ili tupanuane mawazo.

Juzi Raila Odinga - Kiongozi wa NASA nchini kenya aliapa kama "Raisi wa Watu". Hapakuwa na polisi wala mtu yeyote aliyeingilia kati katiak kupasa huko zaidi ya serikali kuzima vituo vya habari kadhaa kuzuia visirushe tukio hilo. Maswali yangu ni:-

1). Katiba ya kenya inatoa mwongozo upi kwa mtu kuitwa "Raisi wa watu"?

2). Huyo Ojwang sijui (mbunge) aliyekuwepo kweney hilo tukio tunasikia kakamatwa jana. Amekamatwa kwa kosa gani?

3). Huyo Raisi wa Watu anafanya jinai gani hadi akamatwe?

Mods, naomba msiunganishe uzi huu na uzi mwingine kwa sababu una makusudi maalumu ya kufundishana sayansi ya sheria.

Ninaomba wanaojua sheria za Kenya, Wachambuzi wa siasa (wa kweli), wanasayansi za siasa na jamii, wadau na waathirika wa "uraisi wa watu" wa Odinga, waje hapa tupeane maarifa.

Kama huna hoja, unaweza kuuliza ama kusoma na kujifunz akwa wengine.

Karibuni.
 
Nakushauri ili tupate majibu sahihi wewe ita watu pale shamba la bibi halafu ujiapishe kuwa rais wa watu ukipelekwa mahakamani watakusomea shitaka halafu utakuja kutujuza kosa lako.
 
Haipo, rais wa watu what does it mean? Mtababaduana sana mahakamani kuonyesha kuwa alikuwa na nia ya kuiondoa serikali iliyopo madarakani.
 
Nakushauri ili tupate majibu sahihi wewe ita watu pale shamba la bibi halafu ujiapishe kuwa rais wa watu ukipelekwa mahakamani watakusomea shitaka halafu utakuja kutujuza kosa lako.

Kama huna jibu, unaweza kusubiri wanaofahamu waje watoe ufafanuzi. Nimetahadharisha mapema. Na nadhani unafahamu kwamba mtu makini hujifunza kwa makosa ya wengine bali mpumbavu husubiri kujifunza kwa makosa yake.
 
Lakini mbowe alisema sisi tupo upande wa kenyata rafiki wa luwassa. kamanda unaleta mambo gani tena hapa
 
Kama huna jibu, unaweza kusubiri wanaofahamu waje watoe ufafanuzi. Nimetahadharisha mapema. Na nadhani unafahamu kwamba mtu makini hujifunza kwa makosa ya wengine bali mpumbavu husubiri kujifunza kwa makosa yake.
sure
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…