Odinga una hoja lakini nina mashaka nawe!.

MLA PANYA SWANGA

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2015
Posts
5,184
Reaction score
5,435
Uchaguzi nchini kenya umetangazwa na tume yao huru na kumtangaza Uhuru Kenyatta kuwa mshindi. Ni sahihi kadri ya takwimu za kura zilizokusanya huko.
Tume hiyo imehusika kutangaza matokeo ngazi zote na wahusika wamesikia.
Mara baada ya ushindi huo Odinga ameenda mahakamani kupinga ushindi huo kwa hoja na ushahidi aliopeleka. Mahakama imetengua ushindi wa Uhuru na kuamuru uchaguzi mpya ufanyike kwa ngazi ya urais tu.
Hapa ndipo ninapopata ukakasi wa hoja ya Odinga kuwa si jasiri bali ni muoga ama anatumia ushauri wa kupewa tu.
Moja :Tume anayoikataa ndiyo hiyo hiyo iliyotoa matokeo ngazi nyingine ambazo wafuasi wake wameridhia na hawajaenda kwa koti. Anataka ivunjwe.
Mbili :Kaingia ktk chaguzi mara kibao na kuambulia patupu akipambana na Mwai kibaki, Uhuru hakuwahi kufanya haya. Ina maana akishindwa uchaguzi tena atasema nini?.
Tatu, :Ikiwa Uhuru akashindwa uchaguzi naye kwa kuwa katiba inamruhusu akaenda koti akapinga matokeo na akashinda uchaguzi utafanyika tena?.
Mwisho :,Katiba ipo lakini inaweza ikavunjwa na isifuatwe na kiongozi aliye madarakani na akatumia ubabe kama ilivyo kwa nchi jirani na kenya hali itakuwaje.

Ni kweli makosa hayakosekani ktk chaguzi zote ila ni vema kukawa na aina ya makosa ambayo yakifanyika lazima uchaguzi kurudiwa hususani yanayohusiana na takwimu.
Uingereza marefa hufanya makosa mengi uwanjani hadi timu husika kukosa ushindi lakini anayeadhibiwa ni tume husika FA, .
Kuna harufu ya ushauri kutoka nje kwenda kwa Odinga ili mradi tu kuhakikisha anaingia ktk migogoro michafu.
Ikumbukwe huyu Uhuru aliundiwa kesi na wakenya wa kisiasa ili Uhuru afungwe na anyongwe lakini Mungu alimnusuru.
Ushauri wangu kwa wakenya msikubali kugawanywa na watu wa nje walioshindwa kuongoza nchi zao. Dunia inajua uchumi wenu ni imara na wanahaha namna ya kuwavuruga ili muwe masikini kwani siku zote tajiri hatawaliki bali masikini.

Mtakuja kukumbuka shuka wakati kumekucha. Angalieni washauri wakuu wa wahusika kisha muwapime wanaongozaje nchi zao.
Ikiwa tume ni mbovu na takwimu si sahihi iweje ngazi nyingine asiappeal ila ya uraisi tu wakati uchaguzi siku moja wasimamizi wale wale na wachaguliwa wale wale?.

Mwisho, iweje aikatae tume ya uchaguzi ila kaikubali mahakama kwa kuwa imetenda sawa na hitaji la moyo wake.

Allow many people to advice you, but do not let them to decide for you let decision be your own property.
Wakenya tunawasihi kama majirani zenu ukabila ni sehemu ya matatizo yenu. Msikubali kugawanywa kwa namna yoyote.
Mimi na familia yangu tunawatakia wakenya wote umoja, mshikamano na afya njema kuelekea uchaguzi mpya tukisema ya kuwa "Tafuteni kuwa na amani na watu wote na huo utakatifu ambao hakuna mtu atakayemuona Mungu asipokuwa nao ".
Mungu ibariki Tanzania, Mungu wakumbuke wakenya, Mungu wakumbuke watu wote duniani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ya kenya waachie wakenya

Hivi kwa nini kila waafika mnachokiharibu mnasingizia wazungu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…