"Offside trap" mbinu inayotumiwa na Barcelona Fc kudhibiti wachezaji tishio duniani, mpaka sasa hakuna kocha mwenye mwarobaini wa kuizuia

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Posts
4,701
Reaction score
11,920
Siku zote falsafa yangu ni akili ikishindwa kutatua jambo fulani basi ujinga au wendawazimu utumike kubuni njia mpya ya kutatua changamoto

OFFSIDE TRAP NI NINI?

Hii ni mbinu mpya inayotumiwa na FC BARCELONA kuharibu shambukizi la wapinzani na kuwapunguza makali washambuliaji hatari duniani kama Kilylian Mbappe.

Mabeki wa Barcelona hujipanga ktk mstari myoofu kwa ustadi mkubwa kwq kuhakikisha mchezaji wa timu pinzani yupo offside, yaani mabeki wite huliacha goli wanasogea mbele kabisa kuhakikisha kwamba mchezaji wa timu pinzani yupo offside

Hii huwafanya washambuliakji warudi nyuma zaidi mwisho wa siku wanajijuta waoo kati kati ya uwqnja πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€


Ukiangalia hii picha utaona wachezaji watatu wa Barca waliopo kulia wanamuangalia mchezaji wa madrid aliye na mpira, huku beki aliye kushoto yule wa nne anawaangalia wenzake.

Mpira kabla haujapigwa wao husogea mbele kisha kumwacha mpinzani akiwa offside ndio huanza kumkimbiza

Hapa utaona mshambuliaji wa Madrid yupo offside na mwenzake

Hii mbinu ikimfanya mbape akutwe offside marq 8 na wenzake mara 4 jumla offside 12 πŸ˜†πŸ˜†

Hawa Barcelona ni kama wendawazimu wao ukiwq unapiga faulo ile mchezaji wa timu pinzani anataka kupiga wao hukimbia mbele na kukuachia goli ufunge, unakuta offside wwpo watu 6 πŸ˜†

Mpaka sasq hakuna kocha mwenye mwwrobaini wa hii mbinu

Wewe kama mdau unaionaje hii mbinu?
 
mbona dawa ipo tena nzuri tu anazuga mchezaji kuwa ameingia offside nyinyi mtamuangalia yeye as target ya offside,punde hiyohiyo anachomoka mchezaji ambae hayupo offside!.. na kama mlibweteka mkijua mpira ataufata alie offside lkn akaufata alie onside basi tambo zake mbili tu mnaweza mkalia kilio!.

tena mkifungwa magori mawili ya hivyo basi mnapoteana!
 
Wakati huo wao wakiwa wanaangalia tu ? Hii hapana
 
Hii Africa haifanyi! Bongo ndiyo kabisa haifai kwa marefa wetu wameza filimbi!
 
Nahisi madrid hawakufanyia kazi kabla ya game, otherwise wangewahukumu sana barca, hii mbinu wabadilishe, kuna picha hapo ukiangalia kawakimbia na kaua mtego wa offside.
Kadri unavyozidi kuwakimbia ndivyo unavyorudi nyuma

Mwisho wa siku walijikuta wapo kati kati ya mstari

Hapa Madrid wanapiga faulo angalia mpira ndio unapigwa haujapaa

Madrid wapo offside watu 6 kwa mpigo

Muangalie refa

Hapo hata kama refa ni tatu malogo anaachaje kuonaπŸ˜†

Halafu hao watatu wa barca ndio wanakimbia kuokoa huku wengine zaidi ya 7 wakilikimbia goli

Hii mkuu ipo kiufundi usichukulie poa

Hapo senegal vs japan
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…