Ofisa elimu wilaya adakwa akinywa pombe saa za kazi

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,575
Mashaka Kibaya,Korogwe
WAKATI mgomo wa walimu ukiendelea kufukuta nchi nzima na Serikali ikijaribu kuuzima, Ofisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Korogwe, anadaiwa kukamatwa kwa tuhuma za kunywa bia muda wa saa za kazi jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Chanzo chetu cha habari kimesema kwamba ofisa elimu huyo alikamatwa saa 5 asubuhi kwenye baa moja maarufu iliyopembezoni mwa barabara kuu akiwa anakunywa pombe ambapo askari walimkamata na kumfikisha kituo kikuu cha polisi wilayani hapa.

Kukamatwa kwa ofisa huyo kumekuja siku moja tangu Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo kuamua kuingia darasani katika shule tatu tofauti na kuamua kufundisha wakati mgomo wa walimu ukiendelea.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Korogwe Julai 31, mwaka huu alilazimika kuingia darasani kwenye Shule za Msingi ya Mbeza ,Bagamoyo na Manundu akifundisha somo la hisabati , ikiwa ni njia mojawapo ya kuwawezesha wanafunzi kusoma baada ya walimu wao kugoma.

Jana, Gambo akizungumzia tukio la kukamatwa kwa ofisa elimu huyo, alisema lilitokana na agizo lake baada ya kupokea taarifa kupitia meseji ya simu ya mkononi kutoka kwa wananchi kwamba ofisa huyo anakunywa pombe baa.
 
Bora kugida pombe asubuiasubui maana serikali yenyewe ilishalewa siku nyingi.
 
Bora kugida pombe asubuiasubui maana serikali yenyewe ilishalewa siku nyingi.

sisi wananchi hatufai na viongozi hawafai iliobaki kila mtu ana lalamika 2 tunategemea nchi itajegwa na Wachina???au wazungu?? hao hawakuja ha kujenga nchi wao wamekuja KUTAFUTA..maisha wakifanikiwa wanaludi kwao sisi kaziyetu ni kulalamika 2 je tunaji2ma kikazi??tuunategemea maendeleo yatatokea wapi?? kwa Style hiyooooo??? tunataka kizi kidogo stalehe sana na wasomi wana acha Fani zao .......
 
Afundishe mpaka Viidudu...................... aonje utamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…