beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), mkoa wa Ilala Dar es Salaam, inamshikilia Hussein Hassani (43), kwa kosa la kujifanya Ofisa wa Takukuru na kutapeli wananchi.
Mbali na kujifanya Ofisa wa Takukuru, Hassani ambaye ni mkazi wa Mbagala jijini Dar es Salaam, pia alighushi kitambulisho namba PCCB 1565 chenye jina la Hussein Mhando, cheo cha Ofisa Uchunguzi Mkuu wa Takukuru.
Akizungumza na waandishi Mkuu wa Takukuru Ilala, Christopher Myava, alisema baada ya kughushi kitambulisho Mtuhumiwa alitapeli watu mbalimbali na kujipatia kipato kinyume na sheria.
Myava ameeleza kuwa baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema kuhusu utapeli huo, waliweka mtego Desemba 12 maeneo ya Pachoto Mwananyamala.
"Tuliweka mtego maeneo hayo lakini kwa bahati mbaya alikimbia na kuacha gari baada ya kuona watu asiowafahamu ambao walikuwa karibu na gari namba T618DMS ambalo alikuwa analitumia," alisema.
Mkuu huyo ameongeza kuwa baada ya mtuhumiwa huyo kukimbia na kuacha gari Takukuru ilifanikiwa kulishikilia na Desemba 16 mtuhumiwa alijisalimisha na kukiri kujifanya Ofisa wa Takukuru na kutapeli wananchi.
Aidha mtuhumiwa huyo alikiri kuchana kitambulisho alichoghushi kwa nia ya kupoteza ushahidi baada ya kuwakimbia maofisa wa Takukuru.
"Wakati tunafanya uchunguzi wa mtuhumiwa huyo kabla ya kumkamata tayari kitambulisho tulikuwa tumeshakitoa kopi," alisema.