Ofisa JWTZ ahofiwa kutorokea Rwanda

Wapo wengi sana sana!!wengine hata ikulu wapo!
 
Harufu ya damu kumwagika naihisi sasa. Hizi taarifa zinatisha.
 
Sijui kwa nini 'kipeperushi' hiki Mtz J.pili kinapenda kukuza suala la rwanda. Kila wiki kagame kagame. Hamna kingine cha kuandika?

We mnyarwanda tutakutrap tu kaa vizuri.
 
Mkuu Nicholas sijuhi sakata hilo kama kuna kitu Taifa letu lilijifunza kuhusu umahili wa PK. Saga nzima hii mbona imekaa kiajabu kidogo, inaigia akili kweli kwamba Admin ya Kigali ingeweza kumu-apprehend jamaa huyo bila ya kupata msaada from within(TZ)? PK na wenzake wengewezaje ku-track movement ya muhusika, au jamaa huyu alikuwa amefungwa a tracking system kwenye nguo zake za ndani au alikapewa saa ya mkononi kama zawadi kumbe ina apps za GPS zinazo shirikiana na mtandao wa ku-roam wa GSM bila ya yeye kutambua kinacho endelea - kumbe makomando wa PK wako mpakani na Tablet/Laptop zao waki-track movements zake zote on a digitised map ya East and Central Africa!! Nalisema hili kama utani vile, lakini tukio hili linaonyesha kwamba Taifa letu lina active moles in higher places from within/out, tuwe makini SANA. Najua Mh.JK ni mwanajeshi makini sana anayejali sana usalama waTaifa letu, lakini na usalama wake nao una-count a MEGA TIMES. Tusijidanganye kwamba vitisho vya PK wenda hikawa ni danganya TOTO, neh - mtu ambaye yuko highly umpredictable kama alivyo PK hapashwi kumchukulia kimzaa mzaa, mambo yanavyo onekana TISS inapashwa kuingilia kati fasta kwa (KU-VET) wafanyakazi wote wanao mzunguka Mh.JK bila ya kujali wadhifa wao save ndugu wake wa DAMU/Nasaba, waende mpaka vijijini kufatilia backgrounds zao kwa kina kama ilivyo kuwa inafanyika enzi za Kambarage, we don't like suprises kama hizi za a high ranking Military officer kugundulika kumbe ni mole wa nchi jirani - hatutaki kushtukia incident kama hizi zikihibuka pale magogoni. Mimi ndio ushauri wangu huo, lakini kadri ninavyo lifahamu TAIFA letu sina shaka kazi hii imekwisha wekwa sawa siku nyingi tu, lakini si mbaya tuki-revisit tena kutokana na current events/situation.
 

Ilikuwaje mkamuachia hadi akafikia Lt. kanali? Tena nyie TISS ndio bure
kabisa, vilaza wakubwa, kazi kujisifia mnapokua baa... matahaira
wakubwa nyie...
 
NI kwa vile tuna kiburi kw akufanya operation ambazo zina limited threat....huku tukiwa na maaudui ambao bado ni wanafunzi wetu au wamebanwa ktk resources na experiences.Ila kwa muda wote PK akiwa nakubalika na mataofa ameweza traian watu wake, kattumia nchi km uganda hata kongo kuleta watuw ake kujifunza kwetu kwa lengo moja la kujipima napengine waipewa unlimitted access ili waweze kwenda kufanya kazi ya TZ na pengine walikuwa walikileta maelezeo fulani ili kusimlate jeshi letu kufany amafunzo yanayokusudiwa zuia threat fulani yao ya uongo ili kujua uwezo wetu wa kukabilia na vitu fulani.


Nadhani tunahitaji mengi sana kulifanya jeshi letu flexible, ingawa watanzania wakifanya maamuzi ya kuiondoa CCM smoothly tutaweza pona na kusafisha jeshi.
 

Mkuu unajua unachokiandika au MP inakusumbua?... Nani kakueleza Lt.
Kanali ni nyota 2, na ukiwa na degree TU, ukianza jeshi unapewa cheo cha
Lt. Kanali....

Si bure utakua na mihemuko....
 
Kumbe wewe unafahamiana naye huyo jamaa? Unajuaje kama aliondoka miezi mitatu ilivyopita? Maana migogoro na Kagame imeanza mwezi wa sita mwanzoni, ina maana wakati migogoro inaanza jamaa alikuwa ameshaondoka? Acha uzushi wewe. Au wewe ni mmojawao hao waliopenyezwa nchini?
 
Kama jamaa wame infiltrate kiasi hiki, ipo siku tutasikia JK amepigwa "Cold blood" pale pale ikulu...

Kwa sababu PK ameshasema anangojea "right time" ili amu-hit JK.... na yule jamaa yuko serious atanii wala hacheki na kima kama kina JK...
 
Huya jamaa Lt kanali atakua na undugu na KOBA na MUKAMASIMBA.
 
Kwani Kagame aliposema anajua where to hit Kikwete mlidhani ana maana gani. Halafu wapo wengi tena katika idara nyeti zote achilia mbali jeshini.
 

hapo kwenye jk ni mwanajeshi ndipo ulipokosea mkuu, jk alitoka jkt akaenda kuwa mwalimu wa katiba ya ccm jeshini, anajua mwenyewe sarakasi aliyocheza akawa kanali.
 
SIO LAZIMA KUCHANGIA KAMA HUJUI KITU,KUSOMA NA KUPITA PIA NI NJIA YA KUFAHAMU (Tafuta commanding order/chain of command uijue hiyo rank)
 
Itabidi Tanzania ikubaliane na hali hii kwa muda mrefu sana, na ni muhimu kuwa na uongozi wa juu ulio thabiti na makini sana katika mambo ya usalama wa taifa. Kwa muda mrefu sana ilikaribisha wakimbizi wa kutoka nchi za jirani na kuwatunza kama raia wa kawaida. Vizazi vya wakimbizi hao ni raia halali wa Tanzania wenye haki sawa na raia wengine, ikiwa ni pamoja na haki ya kuwa maofisa wa jeshi, mawaziri na hata kuwa rais. Sasa hapo ndipo uthabiti wa usalama wa taifa unapoingilia. Nikichukulia mfano wa nchi ya Marekani ambako hata uraia wa kuomba pia unampa mtu haki karibu zote isipokuwa ile ya kugombea uraisi, linapokuja utoaji wa madaraka nyeti yanayowea kugusa usalama wa nchi wanakuwa makini sana, hata kwa raia ambaye babu wa babu yake alizaliwa hapo hapo Marekani. Wana kitu kinaitwa background check ambacho wanakifanya kwa makini sana ili kujua kama mtu huyo akipewa madaraka hayo hataweza kusaliti taifa. Na hata pale mtu ameshapewa madaraka, vile vile kuna kitu kingine kinaitwa security clearance, ambacho ni kikwazo kingine ambacho mtu anatakiwa akiruke ili awezeshwe kupata habari nyeti za kiuslama. Kuna wabunge na maseneta wengi ambao hawana hiyo security clearance.

Ingawa mara kwa mara kunatokea kuwapo kwa uvujaji wa siri kama huo wa Snowden, lakini inatokea kwa nadra mno- Snowden alikuwa mfanyakazi wa kima cha chini kwenye kampuni iliyokuwa imepewa tenda na serikali. Major Nidal Hasan aliyeua wenzake kule Texas alikuwa anaangaliwa kwa makini sana na hata kupandishwa kwake cheo kulifanyika baada ya kushauriana sana ndani kwa ndani kwa vile hakuonekana kuaminiwa vya kutosha. Kutokana na hali hiyo, hakuwa na access na information nyeti kiusalama, yaani hakuwa na security clearance.

Tanzania hapa tumewahi kuwa na hata mkuu wa usalama wa Taifa akiwa ni wa kutoka Rwanda, na hapo ndipo tunapotakiwa kujiangalia tena kwa makini sana kuhusu usalama wa nchi hii. Mtu hawezi kubaguliwa kutokana na wazazi wake walikotokea, lakini vile vile tuamini tena kuwa ni vigumu mtu kuwa na allegiance kwa nchi mbili sawasawa.
 
Na huu ndiyo ujinga siku zote tunaoufanya wa kuajiri bila kuchukuwa hatua ya utafiti wa kina tukiendelea lazima utukosti
 
Huenda wamefanya kazi yao wazee wa kazi hao bana kila kitu kuwahiyana tuu
 
mfumo wetu wa ajira ni mbovu sana. Serikali za mashina hazishirikishwi kabisa. Tulishangaa Kagame anapata wapi kiburi ehe? Majibu yanaanza kuja. Kuna wakili maarufu aliuawa hapa rumours zikamtaja Kagame. Jaribio la mauaji South Afrika ikatajwa tz na Kagame.
 

ALEYN, nadhani wachanganya mambo, huyu sio Luteni (mwenye nyota mbili). Alishapita luteni, capt, major, na sasa ni Luteni Kanali. Huwezi kuanza na cheo hiko na degree yako. Sitaki kuamini kwamba kweli kapotea ba jeshi halina taarifa kama kweli alishakua suspect na intelijensia ya JWTZ, si kila tukio wataliweka wazi kwa wananchi. Amini tu mko salama.
 
Mhe. Kichuguu,

Naona maelezo yako ni mazuri ila kuhusu USA umeenda kando kidogo maana hata Rais wao Obama baba ni mtu wa Kenya.

Mimi kila wakati naeleza kuwa tuna watu wengi sana kutoka nchi za jirani. Tufanye uchunguzi wa kina na kubaini wote bila ya kuacha hata mmoja. Warundi na Wanyarwanda wakiwa watusi au wahutu waondoke pamoja na baadhi yao kujipachika makabila ya Tanzania. Kwa mfano kuna wale wamejipachika kuwa wahaya, wanyambo, wahangaza, washubi, waha na wengine wameitwa wasukuma. Hata maeneo ya Kilimanjaro, Tanga na Dodoma wapo.

Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo (1985-1992) kuna watu walikuwa wanazozana kwenye media yetu ambapo mwandishi alikuwa anamshambulia mtu anayeitwa Chiguyeminsi akimaanisha watu wa Dodoma waliokuja kwa ajili ya kulima Mkonge wakitokea Burundi na Rwanda na baadae kubakia Tanzania wakiitwa Wagogo na makabila mengine ya Tanga. Baadae huyo mwandishi akashughulikiwa kutokana na kuandika na kuwazungumzia waliokuwa wanataka urais mwaka 1995. Hii inaonyesha ukubwa wa tatizo tulilonalo la wahamiaji haramu tuliowakubali bila hata ya kuomba uraia.

Cha muhimu kwa sasa ni kufanya uchunguzi wa kina. Kuhakikisha hakuna anayebaki nchini bila kujulikana na kuwa na uraia utakao base kwenye uzalendo wao siyo kugawa kama njugu kwani hata JK amewapa warundi zaidi ya 162,000 hivi karibuni na hao wote bado wana mawasiliano ya karibu na ndugu zao kiasi cha hata serikali yao kuhisi kipindi fulani kuwa Tanzania inasaidia waasi.

Nachojua itakuwa rahisi kuwabaini watusi wote kurokana na sura zao ila wahutu watajificha sana. Wote waondoke wakaishi kwao na wamalize tofauti zao kama ushauli wa JK alivyoutoa ingawa naye wanasema ana asili ya Burundi.

Anjo
 
Mkuu ALEYN cheo cha Lt Col ni kikubwa sana jeshi na si JWTZ tu bali majeshi yote unayoyajua dunia.Huyu mjeshi kaanzia Lt usu akapanda hadi Lt kamili,then Capt,Major hadi Lt Col lazima kaenda kazi kadhaa za nguvu eg Platoon cammander course (kiongozi wa kikosi cha between 26 - 64) lazima atakuwa amehudhuria course ya Company cammander (kiongozi wa kikosi cha jeshi 80 - 225) halafu atakuwa ana mafunzo ya kuongoza Battalion (kiongozi wa between 300 - 1200) kutegemeana na mfumo wa jeshi au aina ya kikosi eg Artillery units,Logistics units, or air defence and ets au unafuata system gani ingawa inafahamika JWTZ ilikuwa ikifuata mfumo wa China na Russia siku hizi naona Marekani nayo inajiingiza ingiza.

Kifupi Lt Col ni mjeshi wa cheo cha juu sana huyu kabakiza ngazi mbili afikie cheo cha one star general ili aweze kuongoza regiment au brigade.


 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…