Ofisa JWTZ ahofiwa kutorokea Rwanda

Mkuu Nicholas ni kweli kabisa kuna jamaa wakati tunapiga shule chuo mwaka 2002 akanishangaza sana baada ya kuniambia yeye alishiriki vita ya kumwingiza Museveni mwaka 1986 (lazima alikuwa mdogo sana,lazima Museveni alitumia watoto kipindi hicho)Leo yuko Tanzania kila ukipiga story za Rwanda jamaa anamtetea Kagame mpaka utashangaa.Huyu ni raia wa Tanzania mwenye mafunzo ya kijeshi ninavyoelewa mimi mjeshi hapati uraia wa nchi nyingine zaidi ya ile aliyozaliwa na kuitimikia kijeshi.TISS wanashughulika na CDM,Mwanahalisi,Dr Ulimboka hawajui kuna kitisho cha toka nje na ndani ya mipaka yetu.

Wakati tunapigana vita na Idd Amini Tanzania ilikuwa na umoja leo hatuna umoja,udini umetugawanya,ukanda umetugawanya,ufisadi umetugawanya vyama vimetugawanya.Umoja umetoweka !!!!!.Ukiwaamba leo hii wananchi wa kawaida tukapigane vita nchi yetu imevamiwa wengine watauliza kwanza waliochota fedha za meremeta watakuwa mstari wa mbele,waliochota fedha za EPA watatangulizwa msatari wa mbele,waliokula fedha za Radar wana nafasi gani katika kuitetea nchi ?.wanaovuruga amani huku wameshika vitabu vya dini wana nafasi gani katika kuitetea Tanzania.

Ukweli ni kwamba Kikwete na serekali yake wamechezea tunu ya taifa kwa muda mrefu sana.Ni wakati muhafaka sasa nchi ikarejesha misingi ya taifa linaloitwa Tanzania.


 
Last edited by a moderator:
Kikwete ana nini na rwanda???

Matokeo ya kauli za dharau zinaliingiza taifa kwenye matatizo makubwa.


Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

kauli ipi ya dharau aliyoitoa jk dhidi ya rwanda?
 

ss si tunajifanya nchi ya amani na nyenye upendo na watu wote, ngoja tuonje shubiri,

watu wa rwanda wako wengi mno wanegine ni wakuu wa sekondari, wangine wamewahi kuwa mawaziri, wengine wamewahi kuwa wakuu wa vyombo mablimbali vay nchi, wengine wamepewa hadi passport za Tanzania

sio hilo tu hata Kinana KM wa CCM ni raia wa Tz kutoka Somalia au sivyo? mwenyekiti wa ccm mkoa wa Mara sio mtanzania nk. tukumbuke hakuna anayeacha asili yake hata akikana uraia wake. wengine wanaukana kwa maelekezo ya serikali zao kuwa watawatumia katika maeneo fulani ndio maana strategically wanapoingia katika nchi yetu wanakuwa katika maeneo maalumu kabisa

wapo wengine wanafanana kabisa na Kagame lkn wana passport za tz, vyeti vya kuzaliwa vya tz, tumewasomesha kwa kodi za watz, tunatarajia nn?

ukicheka na nyani utavuna mabua,?
 
Ndugu usiogope Mtu mwenyewe kumbe wa IT situnaflsh maprogram yote kijeshijeshi tunaanza upya -Mi ningeogopa sana kama angekuwa mkuu wa pale Ngelengele au Monduli
Duh! wacha ni shushe pimzi
 
Hii ndio Tanzania bwana, Ukachero ni kawaida ndani ya vyombo vya ulinzi mbona sisi tunao wengi tu ndani ya majeshi ya watu. vilevile tunao wanasiasa ndani ya nchi moja hivi kusini mwa tanzania.
 

Nakili kuwa nilijichanganya, JWTZ wapitishe msako mkali. Wakibainika ni Kuwaua tu.
 
Last edited by a moderator:
Sijui kwa nini 'kipeperushi' hiki Mtz J.pili kinapenda kukuza suala la rwanda. Kila wiki kagame kagame. Hamna kingine cha kuandika?
Wengine kama mimi ninapenda sana "kipeperushi hicho". Kwako, usifungue sehemu hiyo wala kusoma!
 
Ukiwa mwanaume legelege mke atakuletea watoto wa nje na kukuambia ni wako ukija shtuka wameishamaliza chuo kikuu na wanajitegemea, Tanzania ni sawa na mwanaume legelege asiyejua majukumu yake...... Ni aibu kwetu sisi wote
 
Mkuu Lukolo mimi jamaa huyu nilishamstukia siku nyingi tu, jaribu kufatilia thread/majibu yake siku za nyuma. Back 2 the point - Taifa letu alikuwahi kuwa na moles kwenye vitengo vyetu nyeti wakati wa utawala wa Habyalimana (MHUTU) na wenzake walio mtangulia (Watutsi); kinacho shangaza kwa nini tangu utawala wa sasa (Rwanda) uingie madarakani naona wako obsessed ku-recruit na pukenyeza moles nchini mwetu wakati hatujawahi kuwa na uhasama/vita na Rwanda na wala hatutegemei kama hilo linaweza kutokea - sasa moles wanapenyezwa kwenye jeshi letu ili iweje, kama ingekuwa upelelezi wa kiuchumi/bihashara ningeweza kuelewa - lakini jeshi? Hii sio dalili nzuri. Kwa akili za kawaida upenyezaji wa moles kwenye JWTZ na Polisi unaweza kutafisiriwa vipi - simple, utawala wa sasa nchini Rwanda hawana/hawakuwa nia njema na TAIFA letu (tangu waingie madarakani) na hii sio kwamba imeanza leo ni long term plan za utawala huu - watu wanafikili uhamiaji holela wa jamaa hawa mkoani Kagera ni bahati mbaya - si kweli, matatizo ya kuchonga nchini DRC (Kivu) wanataka yajirudie Mkoani Kagera.
 
Mkuu NICHOLAS hapa tunazungumzia mambo ya usalama wa Taifa letu, nchi unazo zizungumzia hazijawahi kuvamia nchi jirani na kuondoa watawala madarakani na kuweka wanaowapenda, narudia kupindua Serikali halali au kutishia uhai wa Kiongozi mwenzake - Baba wa Taifa na Mzee Jomo Kenyatta hawakuwa in good terms lakini hatukuwahi kusoma mahali kwamba Kenyatta au Kambarage akimtishia maisha mwezake hata Iddi Amini alizungumzia mambo ya kuingia ulingoni (Ngumi) na Kambarage kama utani. Raia wengi unao wazungumzia hapa ni economic refugees hawana an hidden agenda za kujitanua kwa njia yoyote ile hata kama ni kupigana vita ili watimize malengo yao wako radhi kabisa - watu wengi tishio hili lililo dhahili wala hawalioni!!!!! Hebu niambie ni nchi gani za jirani ziliwahi kuweka/penyeza moles kwenye JWTZ, Polisi kawaida, Uhamiaji and the list goes on. Mkuu Nicholas je nchi jirani kupenyeza moles kwenye vitengo nyeti in peace time kunashiria nini?
 
Mkuu Bukyanagandi, Kagame ana mashaka makubwa sana na Tanzania kwa kuwa ndiyo iliyokuwa msuluhishi wa migogoro yao tangu kabla ya Habyarimana kuuawa. Tanzania inajua vema ushiriki wa Kagame na RPF katika mauaji yale ya kimbali wakati huo akipigana kutokakea Uganda. Unajua ni kwanini Kagame alimuua Prof. Jwani Mwaikusa? Mwaikusa alikuwa na ushahidi wote wa ushiriki wa Kagame kwenye mauaji ya Kimbari. Na wauaji walimuua Mwaikusa na kuchukua tu zile document zake zenye ushahidi na kuishia.
Hata Kikwete anaposema Kagame aongee na wapinzani anajua vema kwamba Kagame ni nani na ameshiriki vipi kwenye lile sakata. Kwa hiyo Kagame amekuwa kama ni mtu wa kujihadhari sana, anaogopa asije akatajwa hadharani.
 
Last edited by a moderator:

Kuondoka kwa huyu Askari kumeniuma sana. Humu ndani Jf kuna Wanyarwanda wengi tu, pole sana kwa kuwajibu Mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Kuondoka kwa huyu Askari kumeniuma sana. Humu ndani Jf kuna Wanyarwanda wengi tu, pole sana kwa kuwajibu Mkuu.
Yah, ninajua wapo wengi sana na wana maneno kwelikweli. Tutaendelea kuwajibu tu hadi mwisho, ili wajue kwamba tunawajua vema.
 
Jamani mbona wanyarwanda wapo tu wengi jeshini,na walishashikwa siyo mara moja mpakani wakiwa na nyaraka za jeshi letu,sasa kwakuwa kuna mgogoro kati yetu na Rwanda ndo hayo yanaibuka,yapo siku nyingi sana.
 
hapo kwenye jk ni mwanajeshi ndipo ulipokosea mkuu, jk alitoka jkt akaenda kuwa mwalimu wa katiba ya ccm jeshini, anajua mwenyewe sarakasi aliyocheza akawa kanali.
Mkuu kuna tofauti gani kubwa kati ya JKT na JWTZ? je JK alistaafu jeshi akiwa na cheo gani? Nani kakwambia vyeo vya jeshi vinatolewa kama njugu au vyeti vya ONLINE!! Sarakasi ninazo zijua za JK niza kucheza BASKETBALL, sasa kama kuna sarakasi za ziada hiyo sijui mkuu.
 

jk hana tofauti na halima mdee kijeshi wote ni makuruta wa jkt, hivi inawezekana mwalimu wa katiba ya CCM jeshini akapanda mpka kuwa kanali.
 
Kumbe ndiyo maana
kajamaa kana kidomo domo sana! Yaani mpaka mamluki anafikia cheyo cha
Luteni Kanali hagunduliki tu?? Naanza kupata wasiwasi na intelijensia ya
JWTZ.
mleta uzi kaja kuwatisha tu mbona hazungumzii wa tanzania walioko katka jeshi la rwanda ambae wa cheo cha juu sasa ni kanali au majasusi wa tz waliopo vyuo vikuu vya rwanda kama malecturers
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…