lifeofmshaba
JF-Expert Member
- Feb 19, 2011
- 867
- 219

alimaliza masomo korea miezi sita iliyopita
Ofisa mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, Fred Kaombwe (28), amejiua kwa kijipiga risasi kichwani baada ya kumkuta mkewe akiwa na mwanamume mwingine katika baa mojawapo mjini Dodoma. Baada ya hapo, Kaombwe inadaiwa alimkimbiza mkewe huyo Vicky Kaombwe (34) na baadaye alimpiga risasi na kumjeruhi sehemu za mbavu.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Elizabeth Masiaga alisema ,Kaombwe alijipiga risasi juzi saa 3.00 usiku katika mtaa wa Madole eneo la Kigamboni mjini Dodoma.
Kamanda Masiaga alisema, Kaombwe alifariki dunia wakati akipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kupatiwa matibabu wakati mkewe Vicky amelazwa katika hospitali hiyo.
Hata hivyo, hali ya majeruhi huyo anayefanya kazi katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohana mjini Dodoma bado si nzuri na Kamanda Masiaga aliahidi kutoa taarifa zaidi mara baada ya kukamilika kwa uchunguzi.
Akizungumza na gazeti hili, mkwe wa marehemu, Thadei Nghwaya, alidai kulikuwa na ugomvi wa kifamilia na kwamba, Kaombwe alijipiga risasi kifuani na si kichwani baada ya kuhisi kuwa amemuua mkewe.
Nghwaya alisema, baada ya vipimo, ilibainika na wataalamu kuwa risasi aliyojipiga Kaombwe ilipitiliza na haikubaki mwilini.
Akizungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa jina, mmoja wa mashuhuda alidai kuwa, kabla ya mauaji hayo Kaombwe alimkuta mkewe akiwa na mwanamume mwingine katika baa.
Alidai kuwa, baada ya hapo, Vicky alikimbilia katika gari lake na kuondoka nalo huku akifukuzwa na mumewe katika gari lingine hadi walipofika nyumbani kwao eneo la Kigamboni.
Shuhuda huyo alidai kuwa, Vicky aliposhuka katika gari kwa lengo la kufungua geti, Kaombwe alikuwa ameshafika akatoka ndani ya gari lake na kumpiga risasi mkewe.
Kaombwe alisafirishwa jana kwenda Tabora kwa maziko.
source: habari leo
MAONI; sasa hapa kuna nafuu gani?
anyway wamama na wadada jamani kuna wanaume ni dhaifu sio vizuri kuchakachua
mali zao, wanaume kujiua kwa ajili ya penzi, inaingia akili kweli
>>>>>>>>>>>HOT POST YA HII MADA
Re: Ofisa Mipango Chamwino ajiua.... baada ya kumshika mke na lijamaa
Bakantanda,
Mie ni mpenzi wa kuangalia Investgestion Discovery (ID) TV. Kwa hayo uliyoyaandika hapo juu, huyu mama LAZIMA achunguzwe kwa uhakika zaidi. Inaonekana kuna njama zilishasukwa ili kummaliza jamaa. Haiwezekani wanaume wawili wanakufa kwa RISASI wakiwa na huyu mama. Panga pangua hapa kuna namna,
Kama kuna watu wa karibu yake hasa usalama wa Taifa, basi huyu POLISI hawezi kabisa kuwa tishio kwenu. Fuatilieni hili tukio hadi kilichotokea hapo kijulikane. Msimuache huyu mama akaja kuuwa mwingine (kama ni kweli anahusika).
RIP Kaombwe,,,,,,,,<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<
NA
>>>>>>>>>>>>>LEONARDO>
Upo sahihi kabisa mkuu, sema kwa tanzania yetu hii sijui kama marehemu atapewa haki yake, mimi nimeumia sana maana alikuwa a very close friend of mine. Cha kupigania kwa sasa ni walau wadogo zake ambao ni yatima wapate mgao wa mali za marehemu Fredy na alizoachiwa na wazazi wake kabla huyu mwnamke ajawadhulumu. Kweli si kila mwanamke wa kuoa.
UPDATED 29.05.2011 new development on the story now police involved <<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<
Originally Posted by Sniper
{Latest news nilizozipata ni kwamba Fredy hajajiua, Fredy ameuwawa na polisi dodoma. Mkumbuke mwizi wa Fredy ni polisi wa dodoma ambaye anasoma Chuo cha St.John, na siku ya tukio mwizi huyo (polisi) alikuwa na Vicky. Fredy alipigwa risasi ya ubavuni, sehemu ambayo ni ngumu sana kwa mtu kujipiga mwenyewe (na sio kifuani kama vyombo vya habari inavyoripoti), risasi iliyomuua Fredy haijapatikana eneo la tukio, simu ya marehemu haijulikani ilipo na Vicky hajapigwa risasi hata moja kama vyombo vya habari vinavyoripoti.
Hii yote inaonesha kwamba habari iliyotolewa kwenye vyombo vya habari na polisi ni ya uzushi na uongo mtupu. Kwakuwa mmoja wa watuhumiwa ni polisi, na Polisi imeanza kwa kutoa habari zisizo za kweli kuhusu tukio zima, Polisi pia hatuwaamini katika uchunguzi wa kifo cha marehemu.
Naomba kama kuna ndugu wa huyo polisi au Vicky wanapita hapa JF muwa taarifu kabisa kwamba maisha yao yako hatarini, Watu wa dodoma wana hasira na uchungu sana na kifo cha Fredy.]
<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<
Originally Posted by Gagurito
ebwana huyu bwana tunaishi nae jilan hapa kitaani, magorofa mengi kikuyu! Huyo mwanamke huyu ni mume wake wa 3 kati ya wa4 kufariki tena kwa kupigwa au kujipiga risasi. Mmoja aliyenusurika mpaka sasa ni chizi, mwili wa jamaa keshasafirishwa kwenda tabora kwa mazishi. Mungu ampumzishe mahala pema!<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<
Hapa sasa patamu, sijui kama INVISIBLE unaweza kusaidi wengine mikono yetu iko mbali na eneo la tukio,
wanajamvi wa DODOMA , tunaomba DATA Tafadhali