BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Aliyekuwa Mkuu wa Polisi (OCD), wa Wilaya ya Siha, Vicent Lyimo amemwandikia barua Rais Samia Suluhu Hassan, akimuomba aingilie kati suala lake ili Jeshi la Polisi limpatie nakala ya hukumu na mwenendo wa kesi ya kijeshi iliyomshusha cheo.
Lyimo anadai mwaka 2016, alifunguliwa mashtaka katika Mahakama ya kijeshi, akituhumiwa kuwaachia watuhumiwa watatu wa mauaji, mashtaka anayodai kuwa alibambikiwa, kwa sababu waliachiwa na mkuu wa upelelezi (OC-CID).
Kwa mujibu wa ofisa huyo, shauri hilo liliendeshwa kwa miaka minne (2016-2019), na Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Polisi (SACP), Yusuph Ilembo na kutiwa hatiani kwa kosa hilo na kushushwa cheo kutoka Mrakibu wa Polisi (SP) hadi Mkaguzi wa Polisi na kuamriwa kustaafu kwa lazima.
“Niliposhushwa kuwa Inspector (Mkaguzi) nilikuwa na miaka 56, wakadai umri wa kustaafu kwa cheo cha Inspector ni miaka 55. Ila walijichanganya kwa sababu PGO (kanuni za Polisi) zinasema ukikata rufaa hukumu na adhabu zinasitishwa kusubiri maamuzi ya rufaa. Hawakupaswa kuniamuru kustaafu wakati rufaa ilikuwa haijajibiwa. Nafikiri hili kosa ndio maana hawataki kunipa hizo nyaraka.
“Kuninyima nakala halisi za hukumu, mwenendo wa kesi na rufaa ni sawa na kunifunga nyuma mikono nishindwe kufanya chochote mbele ya sheria,” alisisitiza ofisa huyo wa zamani aliyehudumu wilayani Siha mkoani Kilimanjaro alipokuwa akizungumza na Mwananchi jana.
Alisema kama walimshtaki na kumtia hatia kwa haki kwa nini wanasita kumpa nakala hizo? Bila hizo hata nikienda mahakamani au mbele ya chombo kingine chochote cha haki, nitakuwa najisumbua maana huo ndio ushahidi muhimu.
Akijibu swali ni kwa nini anahisi alitengenezewa au kubambikiwa kesi, Lyimo alidai kuwa alikuwa haelewani na mmoja wa viongozi wake na ndiye alitumia madaraka yake kumtengenezea kesi na kunyimwa nyaraka ni mwendelezo huo.
Barua aliyomwandikia Rais
Ofisa huyo alisema alimwandikia Rais barua ya kwanza Desemba 12,2022 na akaandika nyingine ya kukumbushia Januari 13,2023 na sasa ameandika nyingine Februari 9,2023 akimuomba aingilie kati apewe nyaraka.
Katika barua hiyo, amemweleza Rais kuwa; “Hata rufaa yake ilicheleweshwa miaka mitatu tangu mwaka 2019 hadi 2021, bila sababu za msingi na sikupatiwa nakala ya rufaa wala sababu za kukataliwa rufaa yangu kinyume cha sheria na Katiba.”
“Hayo yote ni ishara tosha kwamba nilibambikiwa kesi. Pia nimenyimwa haki yangu ya msingi ya kisheria, kikanuni na kikatiba kubisha hodi mahakamani”alisema.
Akifafanua zaidi kuhusu barua hiyo, Lyimo alidai aliwahi kufungua maombi Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Moshi, lakini yalitupwa kutokana na kukosekana kwa nyaraka halisi ya hukumu na mwenendo wa kesi.
Vigogo wa polisi wafunguka
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa akizungumza na gazeti hili kuhusu suala hilo, alisema kuwa hawezi kulizungumzia badala yake atafutwe msemaji wa jeshi hilo.
Kwa upande wake, msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, David Misime alipoulizwa na Mwananchi jana kama analifahamu jambo hilo, hakukanusha wala kuthibitisha zaidi ya kumtaka ofisa huyo afuate utaratibu wa ndani ya jeshi kudai haki yake.
“Kama anaona alionewa afuate utaratibu zilizopo. Kama kweli alikuwa ni askari aliyeiva na mwenye maadili ya kijeshi,” alisema Misime.
MWANANCHI