Ofisa Polisi, Emmanuel Mkilia na wenzake 3 kortini kwa hasara milioni 798.7/-

Ofisa Polisi, Emmanuel Mkilia na wenzake 3 kortini kwa hasara milioni 798.7/-

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
1578379835599.png

OFISA wa Jeshi la Polisi, Emmanuel Mkilia (44) na wafanyabiashara watatu, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka matatu ikiwemo ya kulisababishia jeshi hilo hasara ya zaidi ya Sh milioni 798.7.

Washitakiwa wengine ni Donald Mhaiki (39) ambaye ni mtaalamu wa masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), Abdi Ally (48) na Mohyadin Hussein (56) wote wafanyabiashara, ambao walifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Salum Ally.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon akisaidiana na Wakili wa Serikali, Janeth Magoho alidai washitakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka matatu, ambayo ni kulisababishia jeshi la Polisi hasara, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji fedha.

Katika mashitaka ya kwanza, alidai Machi 19,2013 na Oktoba 18, 2013 maeneo na jiji la Dar es Salaam walisababishia mamlaka (Jeshi la Polisi) hasara ya Sh 798,789,272.

Pia alidai katika tarehe hizo na maeneo hayo ya jiji la Dar es Salaam, washitakiwa hao walijipatia kutoka jeshi la Polisi Sh 798,789,272 kwa kujifanya wameweka mfumo wa taarifa za watuhumiwa waliokamatwa na ambao wanashikiliwa (Arrest and Detention System) kwenye vituo nane na kutoa hati mbili, zilizoonesha kwamba mfumo huo umewekwa kwenye vituo vinne kitu ambacho walijua si kweli.

Katika mashitaka ya utakatishaji fedha, inadaiwa washitakiwa hao walijipatia fedha hizo wakati wakijua zinatokana na kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu. Hakimu Ally alisema washitakiwa hao, hawatakiwi kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza na kutoa dhamana kwa kesi za uhujumu uchumi isipokuwa hadi Mahakama Kuu. Hata hivyo, Wakili Simon alidai upelelezi wa kesi hiyo upo katika hatua za mwisho kukamilika, hivyo aliomba tarehe nyingine ya kutajwa.


Chanzo: HabariLeo
 
Back
Top Bottom