Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
OFISI YA AL JAMIATUL ISLAMIYYA FI TANGANYIKA 1930s/SASA OFISI YA BAKWATA SHEIKH WA WILAYA NDANI YA OFISI YA AL JAMIATUL ISLAMIYYA FI TANGANYIKA
Picha hiyo ya kwanza ingawa imepigwa miaka ya 1930s imebeba historia kubwa sana katika historia ya TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.
Katika picha hii yuko Kleist Sykes, Maalim Mattar, Ali Mwinyi Tambwe, Liwali Ahmed Saleh na Abdul Sykes akiwa mtoto mdogo labda miaka 10 hivi na mwanafunzi wa Al Jamiatul Islamiyya Muslim School.
Historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika haiwezi kukamilika bila ya kuwataja baadhi ya watu waliomo kwenye picha hii.
Nini walifanya watu hawa?
Kleist Sykes ni muasisi wa African Association 1929 na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika 1933 na ndiye baba yao Abdul, Ally na Abbas.
Maalim Mattar hakuwa katika siasa lakini yeye ni kielelezo cha dhulma waliokuja kufanyiwa masheikh wengi na serikali huru ya Tanganyika.
Abdul Sykes yeye ana mengi lakini yatosha tu kusema kuwa alimpokea Julius Nyerere 1952 na alimsaidia kupata uongozi wa TAA na TANU 1953/1954.
Abdul Sykes kadi yake ya TANU ni No. 3.
Historia hii inakaribia sasa miaka 100.
Hapo katika picha ya pili ndipo nilipofika jana kuomba kupiga picha jengo la Al Jamiatul Islamiyya kwa ndani nikajibiwa kuwa hilo ni ombi gumu lakini niliruhusiwa baada ya kueleza kuwa mimi nipo kwenye jengo la Waislam ambalo lilijengwa na babu zangu.
Jengo hili kwa sasa halipo limejengwa jengo hilo unaloliona katika picha hapo chini.
Hii ilikuwa sehemu ya nyuma ya jengo kuu la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.
Hivi sasa shule imetenganishwa kwa uzio na sehemu hii iliyokuwa ya nyuma.
Picha ya kwanza wa kwanza kushoto waliosimama nyuma ni Maalim Mohamed Mattar.