Hagwila
Member
- Apr 18, 2019
- 82
- 99
Umangimeza kwa baadhi ya maofisa wa serikali maofisini, unyanyasaji na upigaji; umerejea kwa kasi baada ya kupigwa stop kwenye awamu ya tano.
Mtumishi mmoja katika ofisi ya DED Magu anayehusika na masuala ya IT, ikiwa ni pamoja kutuma taarifa za malipo yaliyokwisha kuidhinishwa kwenda benki ili wanufaika wapate malipo yao kwa wakati; amekuwa akikalia taarifa hizo kwasababu zake binafsi, matokeo yake malipo kuchelewa.
Mfano hai ni waalimu wamechelewa kupata fedha zao za likizo ya mwisho wa mwaka 2023, licha ya kujaza Vendor Form mapema Novemba 2023; lakini fedha zimewekwa kwenye akaunti zao mwishoni mwa Disemba 2023, hivyo wengi wao hawakwenda likizo maana ilikuwa imebaki wiki moja tu shule kufunguliwa tarehe 08/1/2024.
Mamlaka husika fuatilieni jambo hili.
Mimi Mdau wa Elimu, Magu.