Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
OFISI YA EAST AFRICAN MUSLIM WELFARE SOCIETY (EAMWS) DAR ES SALAAM
Hilo jengo hapo chini ndipo ilipokuwa ofisi ya East African Muslim Welfare Society (EAMWS)kabla ya kupigwa marufuku na serikali mwaka wa 1968.
Katika miaka ya mwanzoni 1960 tulikuwa tunaishi Mtaa wa Lindi mwisho karibu na Mtaa wa Nkrumah.
Ofisi hii ilikuwa mwisho wa Mtaa wa India unapokutana na Mtaa wa Lindi na kushoto kwake tu ni Mtaa wa Nkrumah.
Ndiyo kusema ofisi ya EAMWS ilikuwa jirani sana na nyumbani kwetu na nikipita nje ya ofisi hiyo mara nyingi.
Kumbukumbu yangu ya ofisi hii ni kuona watu ndani wengi wamekaa kwenye meza wakifanya kazi.
Nilikuwa mtoto mdogo nasoma shule ya msingi hivyo sikujua ile ofisi ilikuwa na umuhimu gani kwa Waislam.
Miaka ikaenda.
Ofisi hii ilirejea katika fikra zangu siku moja mwaka wa 1968 niko sekondari nilipoona picha ya ofisi ya EAMWS imetokea kwenye gazeti la Tanganyika Standard ikionyesha askari wako nje wanailinda gazeti likieleza kuwa jumuia hiyo ya Waislam imepigwa marufuku na serikali.
Ilikuwa kawaida ya baba yangu kununua Tanganyika Standard kila siku na kuja nalo nyumbani.
Tanganyika Standard wakati ule haya yanatokea lilikuwa linachapa taarifa nyingi na picha kuhusu EAMWS na mgogoro uliokuwa umezuka.
Lakini akili yangu ya kitoto haikuweza kutafakari uzito wa jambo lile.
Sikujua kuwa ipo siku nitakuja kuhusika sana katika kuandika historia ya Waislam wa Tanganyika nitautafiti kwa kina mgogoro huu na chanzo chake.
Hakunipitikia kuwa nitatafiti na kusoma mengi katika historia hii na nitasafiri kwingi duniani na kuzungumza kwenye mikutano mingi kueleza historia inayofikia karne moja ya Waislam wa Tanganyika.
EAMWS ilipigwa marufuku muda mfupi baada ya kufanya sherehe ya kuweka jiwe la msingi la Chuo Kikuu Chang'ombe kilichokuwa kinajengwa na jumuiya hiyo na jiwe kuwekwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Iko picha ya kumbukumbu ya sherehe hii ya kuweka jiwe la msingi inamwonyesha Julius Nyerere akiwa na Mufti Sheikh Hassan bin Ameir na Rais wa EAMWS kwa upande wa Tanzania Tewa Said Tewa.
Chuo Kikuu hakikujengwa.
Mufti Sheikh Hassan bin Ameir akakamatwa usiku nyumbani kwake Magomeni ndege ilikuwa tayari imetayarishwa na kurudishwa kwao Zanzibar.
Kwa nini haya yalitokea?
Hivi sasa ofisi hii ya EAMWS niliyokuwa nikipita nje katika utoto wangu imekuwa sehemu ya kuuza mitumba na sehemu nyingine ni duka la pilipili bizari kama picha inavyoonyesha hapo chini.
Picha: Jalada alilonipa marehemu Tewa Said Tewa linaloeleza kuvunjwa kwa EAMWS, Picha ya Tewa alipokwenda Hija 1964 na picha ya kuwekwa kwa jiwe la msingi wa Chuo Kikuu.