Ofisi ya Jiji la Dar yatoa mchanganuo wa Mradi wa ufungaji kamera za Usalama Kariakoo unaogharimu Tsh. Milioni 514

Ofisi ya Jiji la Dar yatoa mchanganuo wa Mradi wa ufungaji kamera za Usalama Kariakoo unaogharimu Tsh. Milioni 514

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
TAARIFA YA UFUNGAJI WA CCTV CAMERA
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam katika mwaka wa fedha 2024/2025 ilitenga fedha kwa ajili ya ufungaji wa CCTV Camera katika barabara na maeneo ya Kariakoo kwa lengo la kuimarisha ulinzi na usalama wa biashara katika eneo la Kariakoo na barabara kuu zinazoingia na kutoka katikati ya jiji letu.

Katika jitihada za kuunga mkono dhamira ya Serikali ya kuhakikisha biashara zinafanyika masaa 24 kwa usalama na ufanisi, Jiji la Dar es Salaam limeingia katika mkataba na Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TAMESA) wenye thamani wa shilingi 514,276,986 pamoja na kodi ya ongezeko la thamani kwa ajili ya ufungaji wa kamera za ulinzi katika maeneo husika.

Kupitia mkataba huu, awamu ya kwanza itahusisha ufungaji wa kamera 40 zitakazofanya kazi saa 24 kwa siku, kuhakikisha ufuatiliaji wa hali ya usalama na udhibiti wa matukio ya kihalifu.

Kitovu cha Kamera hizo zitafungwa katika Kituo cha Polisi Msimbazi na katika ukumbi wa Anatougla.

Lengo la mpango huu ni kuimarisha usalama wa wananchi na wafanyabiashara, kuongeza ufanisi wa shughuli za kibiashara, na kusaidia mamlaka husika katika udhibiti wa usalama wa jiji.

Kamera hizi zitasaidia kurahisisha utambuzi wa matukio, kuimarisha ufuatiliaji wa wahalifu, na kutoa ushahidi wa haraka pale inapohitajika.

Tunapotekeleza mpango huu, tunaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha teknolojia hii inatumika ipasavyo kwa manufaa ya wananchi wote.

Tunatoa rai kwa wananchi na wafanyabiashara kushirikiana nasi kwa kutoa taarifa zozote muhimu zitakazosaidia kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yetu.

Kwa pamoja, tunaweza kujenga jiji salama, lenye mazingira bora ya kufanya biashara na kuendelea kukuza uchumi wa taifa letu.

Asanteni sana.
MKURUGENZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM


=========================

Ufafanuzi zaidi wa mradi huo kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabelya:

Cameras ni hatua ya Mwisho baada ya Mchakato mrefu kufanyika kwa kuzingatia coverage. Mkataba huo unahusisha mambo kadhaa yakiwemo:

1. Usimikaji / Ujenzi wa Fiber Optic eneo lote la CBD

2. Savers (Zenye uwezo Mkubwa)

3. Ujenzi / usimikaji wa Mfumo kwanye Control Rooms (Tuna control Rooms Mbili)
4. Networking

5. Modern Back up System

6. Earth works aidha kwa awamu ya kwanza cameras 40 zitafungwa pamoja na supporting Systems.

Kamera.jpg
 
Back
Top Bottom