KERO Ofisi ya Kata Chamazi inakamata akina mama na kuwalazimisha kulipia hela ya taka ya mwaka mzima

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Joined
Nov 28, 2024
Posts
7
Reaction score
9
Habarini wakuu, nina kero kuhusu ofisi za Kata ya Chamazi Magengeni zamani kilipokuwa kituo kidogo cha polisi.

Majuzi wamekuwa wakikamata watu hasa wakina mama wanawachukua na bajaji mpaka kata wanawafungia ofisini wanaambiwa watoe elfu 36 za usafi, ukiuliza kosa unaambiwa hujalipa ada ya taka sh Tsh. 3000

Pamoja na hilo hata kama una risiti za Desemba, January ulisafiri hukuwepo unalazimishwa kulipa ya mwaka mzima na isitoshe unampa mtu mkononi jamaa mnene anaitwa Aziz

Naomba mamlaka hasa manispaa ya Temeke wachukue hatua haraka
 
Huko mkoa wa kagera wilaya ya kyerwa nilienda ofisi ya kata Nyaruzumbura, kuanzia mtendaji wakata , mtendaji wakijiji na Mwenyekiti wa kijiji ,wanakamata watu nakuwaweka Lockup ya ofisini kwa zaidi ya masaa 12 huku wakiwalipisha gharama kubwa sana,kiukweli niliumia .

Ofisi ya mtendaji pia haina usuluhishi inakandamiza watu sana , mtendaji wa kata anaumiza watu wengi pale kwa maslahi ya tumbo lake yaani ukifika huko ofisini unaweza kujutia.

Takukuru wangelioa hili ingelipendeza NIMEFICHUA UOVU JAMII FORUM lakini naona wamelipuuza .
 
Wale hawalipwi mishahara! Ni kubanana na sisi humo humo!
Kama takataka zinasombwa akina mama toeni! 3000 per month ni ndogo mno.
 
Alafu wanafikiri , kuumiza watu ndiyo uongozi , niliumia sana yaani ofisi inakuwa ni sehemu yakuumizia watu wakati ni sehemu ya kuweka suluhu , mtu anaamua kwa mamlaka aliyonayo kukuhumu bila sababu za msingi , Viongozi watambue uongozi ni daraja tu kuna siku utapita ,kabla yako kumbuka alikuwepo mwingine kabla yako,

Pia serikali kuu ipende kuzungukia hizi wilaya chipukizi , wilaya nyingi zinagubikwa na changamoto na manyanyaso kwa wananchi wao ,alafu ni maamuzi yao binafsi hata kituo cha polisi huwezi kukuta wakitesa watu kizembe.
 
Kaka hakuna anaekataa kulipa ada ya taka changamoto ni kuambiwa kulipa ya mwaka mzima inaingia akilini
 
Alafu wanafikiri , kuumiza watu ndiyo uongozi , niliumia sana yaani ofisi inakuwa ni sehemu yakuumizia watu wakati ni sehemu ya kuweka suluhu , mtu anaamua kwa mamlaka aliyonayo kukuhumu bila sababu za msingi , Viongozi watambue uongozi ni daraja tu kuna siku utapita ,kabla yako kumbuka alikuwepo mwingine kabla yako,

Pia serikali kuu ipende kuzungukia hizi wilaya chipukizi , wilaya nyingi zinagubikwa na changamoto na manyanyaso kwa wananchi wao ,alafu ni maamuzi yao binafsi hata kituo cha polisi huwezi kukuta wakitesa watu kizembe.
Mkuu wangu hapa chamazi ni familia ya kambare kila mtu ni tembo wanakamata watu majumbani kwao na mgambo wanawatishia polisi na wala hawawapeleki mfano juzi wamemkamata mdada anaumwa Ulcers na katoka hospital na dawa zake wamemfungia ndani toka saa 4 mpk saa 10 akazidiwa aka collapse wakampeleka hospitali wakatoa elfu 60 issue hiyo imetokea na hata wakitaka mashaidi mm nikiwemo nitakuja
 
Poleni kama mko mjini na bado changamoto hazifanyiwi kazi basi serikali yetu ndo yenye shida haswa , Kule Kagera Wilaya ya Kyerwa nilichokutana nacho ni hatari zaidi .
 
Back
Top Bottom