Ofisi ya Kurugenzi ya Mwendesha Mashtaka Nchini inafaa iundwe upya

Ofisi ya Kurugenzi ya Mwendesha Mashtaka Nchini inafaa iundwe upya

DATAZ

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2012
Posts
3,799
Reaction score
10,196
Hii ni moja ya ofisi au Taasisi nyeti Sana lakini inayoitia serikali aibu kubwa Sana. Ukiangalia kesi nyingi zinazoendeshwa na waendesha mashtaka wetu utaona yafutayo:-

- nyingi serikali au jamhuri hushindwa kutokana na ushahidi mbovu. Kwa maana ya upelelezi wa kulipia lipua, au wa kubambika na usiofanyiwa utafiti wa kutosha.

- Washitakiwa wengi wanabambikiwa kesi au kusoteshwa kwa muda mrefu mahabusu, kutokana na upelelezi usiokamilika. Na wengine hata Kama huja kuachiwa huru, huwa tayari wamepata madhara makubwa.

- Ofisi ya DPP imekuwa chombo Cha kutweza na kunyanyasa watu ambao wengi wao hawana hatia.

USHAURI.

Ofisi ya DPP inapaswa kuwa chombo huru Kama ilivyo kwa CAG na kiendeshwe na wataalam wenye uweledi na maadili. Aidha Ofisi hii inapaswa kupewa vitendea kazi vya kutosha ili kutekeleza wajibu wake kwa kasi na viwango.

Ofisi ya DPP iache kutumika kisiasa na kufanya mambo kwa malengo ya kisiasa. Kwani hata katika ripoti ya CAG ya hivi majuzi, ilionesha pesa ilizokusanya kwenye plea bargain, ziliishia katika mifuko ya watu!
 
Hii nchi inahitaji Katiba Mpya tu ya Wananchi. Hii iliyopo imeundwa ili kuilinda CCM na watu wake wachache. Na siyo wananchi walio wengi.
 
Mbowe aliachiwa mkashangilia mkasema mahakama imetenda haki.

Dunia nzima inajua Mbowe ni gaidi alitaka kuilipua nchi bila hekma za serikali alikuwa ni life sentence.
Taarifa za Mbowe kuilipua nchi ulizipata kwa mamako au kwa Mumeo?
 
Ila Bavicha, mlikua mnasema sabaya anawabaka 30 kwa siku. Kweli wanaume 30 mnabakwa na mtu mmoja?
 
Back
Top Bottom