The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Khamis Hamza Khamis ametoa wito kwa jamii kuendelea na jitihada za utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti ili kuhakikisha idadi ya miti inaongezeka na kutengeneza misitu itakayosaidia kutunza afya ya udongo na kuwa chanzo cha upatikanaji wa mvua.
Naibu Waziri Khamis ameyasema hayo katika uzinduzi wa programu ya upandaji miti ambayo imefanyika katika Shule ya Sekondari Hazina Jijini Dodoma, ambapo amewasihi wanafunzi na wananchi kushikamana na kuendelea kupanda miti katika maeneo yao.
Aidha, Naibu Waziri Khamis amesema kuna umuhimu wa kuendelea kutoa elimu kwa jamii ili kurithishana elimu ya upandaji miti kwa vitendo ili kusaidia vizazi vijavyo.
Jumla ya miti 500 imepandwa katika Shule ya Sekondari Hazina kupitia kampeni ya Msitu wa Mama.