Mimi nadhani Serikali ingehakikisha kwamba siyo tu wanajenga ofisi za kila mbunge, lakini pia wanaweka samani zote ndani ya ofisi hizo ili mbunge asiwe na sababu ya kununua samani zake mwenyewe au kujenga ofisi mwenyewe. Lakini kwa mazingira haya ambapo wabunge wanajinunulia samani za ofisi zao, hata mimi ningeondoa samani zangu baada ya kushindwa ubunge, hasa ukizingatia mchakato wa kuwania ubunge si wa kirafiki bali ni wa uadui, ugomvi, matusi na kukashifiana baina ya wanaogombea. Kwa nini mtu umwachie "adui" yako vitu ulivyonunua kwa fedha zako mwenyewe, na si Serikali iliyonunua?