Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam imeandaa bonanza maalum lijulikanalo kama Dar es Salaam Standup Bonanza kwa lengo la kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2024.
Bonanza hilo limeandaliwa kwa ubunifu wa kipekee, likiwa na burudani, michezo, na hotuba mbalimbali zenye lengo la kuwahamasisha wananchi kuelewa umuhimu wa kushiriki katika zoezi hilo la kidemokrasia.
Mgeni rasmi wa bonanza hilo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Albert Chalamila, ambaye aliwakilishwa na Katibu Tawala wa Mkoa, Dkt.Toba Nguvila. Katika hotuba yake, Mheshimiwa Nguvila alisisitiza umuhimu wa wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili kuchagua viongozi waadilifu watakaoleta maendeleo katika maeneo yao.
Aidha Dkt.Toba Nguvila amesema kuwa imekua fursa muhimu kwa wananchi wa mkoa huo kupata elimu na kutambua umuhimu na nafasi yao kwenye kumchagua kiongozi anayewafaa kwa maslahi yao na taifa kiujumla.
Wananchi wa Dar es Salaam wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika bonanza hilo na hatimaye kwenye uchaguzi wenyewe, ili kufanikisha azma ya kujenga jamii yenye ushirikiano