Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera ni mabingwa wa kupotosha historia

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera ni mabingwa wa kupotosha historia

ichumu lya

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2016
Posts
2,651
Reaction score
2,790
Historia hii ya Wahaya na Wanyambo ina ukweli gani?[emoji1427]

Je, ni kweli % kubwa ya wanakagera hawakwenda shule?

[emoji1427]
Kama kuna upotoshwaji kwanini Wanakagera tumekaa kimya?
[emoji1427]
Wakati wa Tetemeko la ardhi nikweli serkali ilichangisha fedha kusaidia wahanga?
[emoji1427]
Nimekuwa nikifatilia jambo hili kwa muda sasa nataka kujua ili tuweke historia sawa.
[emoji1427]
Baada ya vita vya Iddi Amin mwaka 1979 nikweli Wanakagera waliiba mifugo ya Waganda na kuileta Tanzania?

Maswali aya yamechangiwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera kupotosha kwa makusudi historia ya Wahaya na Wanyambo. Naomba tusaidiane kuweka kumbukumbu sawa ili kizazi kijacho kipate ukweli.

Kumbuka kuna mambo ya msingi yaliyotikisa uchumi wa Kagera lakini mwandishi kayaficha.

1. HIV
2. Ukame /Njaailiyoitwa (Ibambura mabati)
3. Mafuriko
4. Wakimbizi
5. Vita=1978


[emoji1427][emoji1427][emoji1427][emoji1427][emoji1427][emoji1427][emoji1427][emoji1427][emoji1427]
''Mkoa wa Kagera
WilayaUgandaKm²

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kagera
Kagera
Mkoa wa Kagera

Mahali pa Mkoa wa Kagera katika Tanzania
Majiranukta: 1°55′S 31°18′E
Nchi Tanzania
Wilaya 7
Mji mkuu Bukoba
Serikali
- Mkuu wa Mkoa Meja General Marco Gatitu
Eneo
  • Mkoa 40,838 km²
  • Bara 28,953 km²
  • Maji 11,885 km²
Idadi ya wakazi (2002)
- 2,003,888
Tovuti: Mwanzo
Mkoa wa Kagera kati ya mikoa 31 ya Tanzania ndio mkoa wa kaskazini-magharibi kabisa wenye postikodi namba 35000 [1].. Jina lake linatokana na mto Kagera.

Mkoa wa Kagera umepakana na Burundi, Rwanda na Uganda upande wa Magharibi na Kaskazini. Upande wa Kusini umepakana na mikoa mingine ya Tanzania ya Kigoma, Shinyanga na Geita.

Eneo lake ni km² 28,953 za nchi kavu na km² 11,885 za maji ya ndani, hasa ya Viktoria Nyanza, jumla km² 40,838.

Mkoa wa Kagera uko mnamo mita 1000 juu ya uwiano wa bahari.

Makao makuu ya mkoa ni mji wa Bukoba.

Kiutawala eneo la mkoa limegawiwa kwa wilaya saba: Bukoba, Misenyi, Muleba, Karagwe, Ngara, Biharamulo na Kyerwa pamaoja na eneo la manisipaa ya Bukoba. Misenyi ni wilaya mpya iliyoanzishwa mwaka 2007 na Kyerwa ikafuata mwaka 2012.

Sensa ya mwaka 2002 imeonyesha idadi ya wakazi kuwa 2,003,888 inayoendelea kuongezeka asilimia 3.1 kwa mwaka.

Mkoa huu una makabila makubwa mawili ambayo ni: Wanyambo na Wahaya. Wanyambo huishi kwa wingi wilaya ya Kyerwa na Karagwe na Wahaya huishi kwa wingi wilaya ya Bukoba vijijini na Bukoba mjini. Makabila hayo hupenda kula ndizi kwa wingi.

Asilimia kubwa ya Wanakagera wanafuata mila na desturi za mababu: Mnyambo/Mhaya walikuwa hawawezi kuoana na hiyo bado ipo kwa kiasi kidogo.

Pia mkoa huu una wakimbizi wengi, kwa asilimia kubwa wanatokea nchini Rwanda na Burundi wakipitia wilaya ya Ngara.

Historia ya mkoa
Mkoa huu unapatikana ukanda wa ziwa Viktoria. Katika mkoa huu kuna mambo mengi ambayo yalitetemesha nchi ya Tanzania. Mambo hayo ni pamoja na vita ya Uganda na Tanzania, vita ambavyo vilihusishwa na mkoa huu; ilikuwa mwaka 1978.

Ndipo Idd Amin Dada aliyekuwa Rais wa Uganda alipoliamru jeshi lake kuvamia mkoa wa Kagera. Walianza kuvamia wilaya ya Missenyi. Hapo Julius K. Nyerere aliyekuwa rais wa Tanzania aliamuru jeshi lake kufukuza wavamizi hadi kuvamia nchi ya Uganda.

Agizo hilo lilikuwa zuri lakini vijana wa mkoa wa Kagera walipata shida kwa sababu walilazimishwa kufuzwa Uanamgambo mara moja na kupelekwa vitani. Walipoanza tu vita hivyo raia wa Uganda walishirikiana na jeshi la Tanzania kufichua maficho ya jeshi la Uganda. Jeshi la Tanzania liliwapiga na kuwapora mali zao, vifaa vya kivita na kuwateka wanajeshi wao.

Mwanzoni mwa mwaka wa 1979 Idd Amin Dada alikimbia na Tanzania kushinda vita hivyo. Mara baada ya vita hivyo Watanzania walichukua mali za Uganda, hasa mifugo, na walipofika nchini Tanzania walifurahia na kusherekea ushindi huo.

Mwaka 1996 meli ya MV Bukoba ilizama ikisafirisha abiria kutoka mkoa wa Kagera kwenda Mwanza; watu wengi walikufa na lilikuwa pigo kwa serikali, kwa ndugu na majonzi makubwa kwa Watanzania kwa ujumla. meli hiyo ilikuwa ina mkoani mwanza katika ziwa la victoria

Katika mkoa huohuo mwaka 2016 lilitokea tetemeko la ardhi lililoleta maafa makubwa: watu walikufa, wengine walipoteza mali zao, hususani majumba yao. Uongozi wa mkoa wa Kagera uliomba kila Mtanzania kuchangia angalau shilingi 100 na kuwasaidia.

Jiografia
Hali ya hewa ni nzuri kwa kuishi, kilimo, uvuvi. Mkoa huo ni maarufu kwa ulimaji wa kahawa, ndizi, miwa na chai.

Pia una mbuga za wanyama na umezungukwa na mto Kagera.

Elimu
Katika mkoa huu elimu bado haijaenea kwa watu wote walioko vijijini. Elimu inakua kwa kasi ndogo na watu wengi wa mkoa huu hawajasoma: wengi wanafanya kazi ya kulima. Hali hiyo hufanya taifa kurudi nyuma kimaendeleo maana taifa kama taifa huongozwa na wasomi ili kukua kiuchumi.

Majimbo ya bunge
Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:

Biharamulo : mbunge ni Oscar Rwegasira Mukasa (CCM)
Bukoba Mjini : mbunge ni Wilfred Lwakatare (Chadema)
Bukoba Vijijini : mbunge ni Rweikiza Jasson (CCM)
Karagwe : mbunge ni Innocent Luugha Bashungwa (CCM)
Kyerwa : mbunge ni Innocent Sebba Bilakwate. (CCM)
Muleba Kaskazini : mbunge ni Charles Mwijage ((CCM)
Muleba Kusini : mbunge ni Prof. Anna Tibaijuka (CCM)
Ngara : mbunge ni Alex Gashaza (CCM)
Nkenge : mbunge ni Diodorius Kamala,,.
 
Ngara umeitaja kama wilaya na mbunge wao na kuna wahangaza ambao mimi nilifikiri ni kabila,lakini kumbe makabila ni mawili tu,wahangaza hawamo katika makabila ya Kagera?
 
Ngara umeitaja kama wilaya na mbunge wao na kuna wahangaza ambao mimi nilifikiri ni kabila,lakini kumbe makabila ni mawili tu,wahangaza hawamo katika makabila ya Kagera?
AJABU, hata Wasubi wanao tokea wilaya ya Biharamulo na wenyewe hawajatajwa, how?
 
Vikabila vidogovidogo ni chimbuko lisilo na mizizi mikubwa kwahiyo ayo makabila niliyotaja ndiyo makabila makuu likiongozwa na Wahaya ambao ni %60 mkoa mzima.
 
Nilijitahidi kuweka historia vizuri lakini ukurasa wangu ulifutwa na Mods.
 
Nilijitahidi kuweka historia vizuri lakini ukurasa wangu ulifutwa na Mods.
Wahusika wasilichukulie kabisa hili andiko lako km Historia kwani lina mapungufu mengi na Uongo km vijana/Mgambo wa Kagera walilazimishwa kwenda mafunzoni hatimaye wakaenda vitani kuonesha walipojificha askari wa Idd Amini
Agizo hilo lilikuwa zuri lakini vijana wa mkoa wa Kagera walipata shida kwa sababu walilazimishwa kufuzwa Uanamgambo mara moja na kupelekwa vitani. Walipoanza tu vita hivyo raia wa Uganda walishirikiana na jeshi la Tanzania kufichua maficho ya jeshi la Uganda. Jeshi la Tanzania liliwapiga na kuwapora mali zao, vifaa vya kivita na kuwateka wanajeshi wao.
hapa ndipo UONGO ulipoukoleza
Mara baada ya vita hivyo Watanzania walichukua mali za Uganda, hasa mifugo, na walipofika nchini Tanzania walifurahia na kusherekea ushindi huo.
naona kwa umri hukuwepo, acha tulikuwepo tukiondoka ndipo muunganishe uongo wenu, Idd Amini hakuondolewa na wana Kagera
 
Wahusika wasilichukulie kabisa hili andiko lako km Historia kwani lina mapungufu mengi na Uongo km vijana/Mgambo wa Kagera walilazimishwa kwenda mafunzoni hatimaye wakaenda vitani kuonesha walipojificha askari wa Idd Amini

hapa ndipo UONGO ulipoukoleza

naona kwa umri hukuwepo, acha tulikuwepo tukiondoka ndipo muunganishe uongo wenu, Idd Amini hakuondolewa na wana Kagera
Yaani huyu mleta mada aeleweki historia ipi ya Kagera anaandika. Kuna wilaya ya Muleba na Biharamuro hata Ngara haelezi wakaazi wake ni kina nani? Huu uzi ulitakiwa ufutwe kwa sababu unapotosha. Andiko lina mapungufu mengi.
 
Yaani huyu mleta mada aeleweki historia ipi ya Kagera anaandika. Kuna wilaya ya Muleba na Biharamuro hata Ngara haelezi wakaazi wake ni kina nani? Huu uzi ulitakiwa ufutwe kwa sababu unapotosha. Andiko lina mapungufu mengi.
inaelekea bado mdogo sana kiumri ni hawa waliozaliwa miaka ya 2000 wakakuta majigambo ya NSHOMILE basi na hivi hajatoka nje ya Kagera amejua Dunia yote imeanzia hapo. Watanzania kwa makabila yote wapo Kagera, na wameathirika kwa Vita, Gonjwa letu lile na hata tetemeko. hii HISTORI ISIPOKELEWE naunga mkono
 
Hilo la kuiba mifugo na kutosoma na uongo
 
Back
Top Bottom