TAARIFA KWA UMMA - ni umma upi ambao haujui hata taratibu za kupitisha miswaada ya sheria Bungeni na baadae kuwa Sheria??? Sasa yaonekana kana kwamba Umma ndo umafundishwa ili uamini yale ambayo Mwanasheria Mkuu (Serikali) inataka wayajue hata kama sivyo ndivyo!.
Tarehe 17 Machi, 2010, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete alitia saini Muswada wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi na hivyo Muswada huo kuwa Sheria Kamili- Kama Muswaada kabla ya kutiwa saini na Rais huwa sio Sheria, ni vipi unakuwa "Sheria Kamili???"
Hivi karibuni, Mheshimiwa Dk Wilbrod Slaa alitoa madai kwamba kuna kifungu kidogo cha (3) ambacho kimeingizwa katika kifungu cha 7 cha Sheria hiyo isivyo halali au "kinyemela". - Je, vifungu vingine katika Sheria hiyo vimewekwa kwa kuzingatia utaratibu sawa na hicho kinacholalamikiwa kama sivyo, basi jibu ni kukubalina na Slaa kwani uhalali ni kuzingatia utaratibu, vinginevyo ni kama kulizunguka Bunge kwa kwa kuomba lipitishe Mswaada ambao baadae unaanza kucheza nao kwa utashi wako na si kwa kuzingatia maamuzi ya Bunge ambayo yamo pia kwenye rekodi za Bunge (Hansard).
Mheshimiwa Dk. Slaa anadai kwamba kifungu cha 7(3) hakikuwepo kabisa kwenye Muswada wa Sheria uliojadiliwa na hatimaye kupitishwa na Bunge = hoja ya kubishaniwa hapa ni Je, kilikuwepo tarehe ambayo Bunge lilipitisha Muswaada?? (Muswaada uliposomwa kwa mara ya tatu kifungu kwa kifungu na wabunhge wote kuridhia??), Je, rejea kwenye Hansard inasemaje kuhusu kifungu hiki?.
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inatoa Taarifa kwa Umma yenye lengo la kufafanua kile kilichotokea Bungeni hususan uandishi wa kifungu cha 7(3) katika Sheria ya Gharama za Uchaguzi - Kwa nini ufafanuzi usiwe kwa vifungu vyote na iwe kwa hicho kinachobishaniwa tu kama kweli utaratibu wa kukingiza ulizingatiwa???
Baada ya Muswada huo kuchapishwa kwa mara ya pili, kifungu cha 7 hakikuwa na vifungu vya (1), (2) na (3). Hata hivyo, kwa kuzingatia hoja zaidi zilizotolewa na Wabunge kuhusu makundi ya Sanaa na Viongozi wa Vyama wanaoweza kumsaidia Mgombea wakati wa Kampeni za Uchaguzi, Serikali kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Sera na Uratibu wa Bunge) Mhe. Philip S.Marmo, iliandaa Jedwali la Marekebisho ambalo lilifanya marekebisho katika kifungu cha 7.- Marekebisho hayo ni:
(a) kukitaja kifungu cha 7 kilichokuwepo kuwa kifungu kidogo cha (1) katika kifungu hicho hicho cha 7.
(b) kuongeza kifungu kidogo cha (2) ili kuongeza makundi ya sanaa na kundi la watu wanaoweza kufadhiliwa na Mgombea kwa chakula, vinywaji, malazi na usafiri wakati wa Kampeni za Uchaguzi. - Je, marekebisho husika waliyowasilishwa na Waziri yaligusa pia kifungu kidogo cha 7(3) ??Kama jibu ni hapana, Je, tukisema Muswaada uliopitishwa na Bunge sio huo ambao umesainiwa na Rais haitakuwa sahihi kama inavyodaiwa na Dr. Slaa??
Kwa kuwa uamuzi huu ulifanyika wakati wa Kamati ya Bunge Zima, Mwenyekiti aliagiza kwamba suala hilo la kuweka marekebisho hayo, lizingatiwe wakati wa kutoa tafsiri ya maneno "timu ya kampeni". Kwa kuzingatia mapendekezo ya Mhe. William H. Shellukindo kwamba idadi ya timu ya kampeni itazamwe na iwekwe wazi badala ya kuiacha wazi tu. Katika kutekeleza hayo, kifungu kidogo cha (3) kiliongezwa kwenye kifungu cha 7 cha Muswada wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi, ambapo tafsiri ya msamiati "Timu ya Kampeni" iliwekwa katika kifungu ambacho msamiati huo umetumika. Hii ndiyo sababu kifungu kidogo cha (3) kiliongezwa.- Je, kifungu kinachohusu tafsiri ya maneno (Interpretation Provision) kinahusianaje na kubadilisha vifungu vya ndani vya Sheria tena kwa kuongeza kifungu kipya???.Je, ikitokea ubishani wa tafsiri ya Kifungu hicho kilichoongezwa (rules of interpreation)katika kupata maana halisi ya nia ya Bunge (intention of the Parliament),je hivyo kinavyosomeak asas ndivyo Bunge lilivyotaka kiandikwe, au tafsiri inatokana na nia ya Mwanasheria Mkuu (Intention of the Attorney General ) na sio ya Bunge??
Iwapo hoja toka kwa Mhe. W.H. Shellukiondo (Mb) ilihusu kutazamwa upya timu ya Kampeni ilitolewa Bungeni wakati Muswaada haujapitishwa (kwa maana ya kusomwa kwa mara ya tatu), je, kwenye jedwwali la marekebisho (schedule of Amendments) lililowasilishwa na Waziri husika kabla ya Bunge kuridhia Muswaada wa Sheria, kwa nini kifungu cha 7(3) halikutajwa kuwa kimeongezwa ili Wabunge wajue na kuridhia kwa pamoja marekebisho husika???
Kwa kuzingatia taaluma ya uandishi wa sheria ilibidi kuongeza masharti yenye amri ya kisheria (Legislative rules) katika kifungu hicho ili tafsiri ya "Timu ya Kampeni" ijitosheleze. Masharti hayo ni yale yanayohitaji uthibitisho wa watu waliomo katika "Timu ya Kampeni". Kwa maelezo haya ni dhahiri kuwa, kifungu cha 7 kilirekebishwa na kupitishwa na Bunge -Kama ofisi ya Mwanasheria Mkuu itatumia taaluma ya Sheria kurekebisha Sheria hata nje ya yale yaliyopitishwa na Bunge, kwa nini tusiamini kuwa ofisi hii nyeti imechukuwa madaraka ya Bunge ya kutunda Sheria badala ya kuandika na kuwasilisha Miswaada ya Sheria ili Bunge ipitisha kadri ambavyo Bunge limeiagiza???
Huu ni utaratibu uliozoeleka wa kutekeleza maelekezo ya Bunge katika Mazingira ambayo Bunge linakaa kama Kamati ya Bunge Zima. -Kama huu ndo utarataibu uliozoeleka, kwa nini tusiamini kuwa Miswaada yote inayopitishwa na Bunge huwa badae inafanyiwa tena nyongeza na Ofisi ya Mwansheria Mkuu kabla ya kutiwa saini na Rais kuwa Sheria jambo ambalo Bunge haliwi tena chombo cha kutunga Sheria na badala yake linaelekezwa na kuridhia yale waandishi wa Sheria wanayoyajua kwa taaluma yao. Na ikiwa Mswaada unaweza kurekebishwa kwa kuongezwa vifungu kwa jinsi hii, kuna haja gani ya miswaada kuwa inasomwa zaidi ya mara moja Bungeni kabla ya kupitishwa kuwa Sheria??? na kwa nini kama ofisi ya Mwansheria Mkuu iliona ipo haja ya kuwa na nyongeza ya kifungu katika kifungu cha 7 isingesubiri kuwasilisha tena Bungeni Mswaada wa marekebisho (Miscellenous Amendments) badala ya kujiamuliwa tu kuongeza hata yale ambayo pengine Bunge lisingeyakubali eti kwa kuwa ni uzoefu???
Hapa utata tupu!