Ofisi ya Mwanasheria Mkuu yapangua hoja ya Dr. Slaa

Wandugu tatizo la maelezo ya Mwanasheria Mkuu liko wapi?................naomba mnielimishe............
Nilivyomuelewa AG.......amesema kulingana na utaratibu wa Bunge AG akisha draft......inarudishwa Bungeni kuridhiwa..........au?


Pia ukipitia hansard hili jambo linaeleweka.......au?

BTW: Hivi wewe Chenge pamoja na ndondo zako zote hizo.........ilikuwaje ukatuingiza mikengeni (mikataba mibovu na manunuzi ya hovyo) namna ile............yaani naendelea kuridhika kuwa wewe ni FISADI kweli kweli.............damn
 
Wote hapa mnaongea kishabiki sana Hoja ya Dr'.Slaa ina hoja muhimu sana cha msingi hapa kama waliongeza kipengele chochote kile
 
Buchanan,Approval itoke wapi sasa? Ujue Tume yetu ya Taifa ya Uchaguzi haina maofisa wake katika ngazi yoyote ile ya chini kama mkoa, wilaya, jimbo au kata. Tumwamini AG wetu. Ni mtu makini sana ingawa sio malaika.

Suala la approval halijaongelewa Bungeni ndugu na ndio hoja ya msingi ya Dkt Slaa! Huoni hapa AG amepiga chenga ya mwili, hakuongelea hata kidogo Schedule of Amendments ambazo hazina mambo ya Approval, amezungumzia tu hoja za Shellukindo ambazo hazijibu hata kidogo hoja za Dkt Slaa! Nafikiri umeelewa sasa!
 
Maelezo ya AG yamejitosheleza mengine yatabaki kuwa kazi za wanasiasa.
Bravo AG!
Si lazima uwe mwanasheria ili uweze kutunga sheria, lakini ni lazima uwe mwanasheria ili uweze kuandika sheria.

Hebu onesha ni wapi kwenye Hansard mambo ya Approval yaliongelewa Bungeni wakati wanajadili kifungu cha 7 cha Sheria za Gharama za Uchaguzi, 2010, Na. 6 ya 2010, kisha umpe Bravo AG kama atakuwa anastahili!
 
Nimekukubali mkuu. Hakuna popote walipokubaliana kuwa pawe na mtu wa ku-approve campain team! Na hii ndiyo hoja ya Dr. Slaa. Wao walichosema ni kudefine campain team kwenye interpretation. Suala la kuapprove, lingepaswa kujadiliwa upya kwani ni ku-establish approving authority ambayo nayo ingewekwa kwenye interpretation na kutaja hao waliowekwa na mwanasheria; inawezekana wabunge wangewakubali au wangewakataa, Kuwaweka hao makatibu tarafa nk hakukujadiliwa na bunge wala kukubaliwa na bunge hata by implication; NI NYONGEZA YA MWANANSHERIA TU.
 
WildCard,
Ni kweli unasema tuache ianze kazi kwanza. Sababu yako ni kuwa kuna sheria nyingi mbovu. Nadhani, huja hapa siyo tu kuwa Sheria hii ni mbovu. Tofauti na Mwanasheria Mkuu wa Serikali alivyojipiga piga hapa, Tatizo ni kuwa dhana ya "Approving Authority", ni dhana mpya kabisa. Vinginevyo, kama Legislative rules zinataka hivyo hakuna sababu ya kuwa na Bunge kwa sababu Serikali ingeliweza kusikiliza tu Bunge, na kwenda kuyaweka maneno wanayotaka kuweka wao. Bunge ndio linalotunga Sheria Siyo Serikali. Hivyo, hakuna ruksa kwa wakati wowote ule dhana mpya kuingizwa kwenye Sheria, vinginevyo Serikali kama inaiingiza dhana mpya ilitakiwa kuleta tena sheria hiyo Bungeni.
Pili, WildCard, kwa mtu anayetaka kujua, madhara yako dhahiri. Kampeni Team ni chombo cha mgombea. Siri zote za ushindi zinatokana na mipango safi na sahihi inayowekwa na Kampeni Team. Hivyo, huwezi kuweka mamlaka ya kuthibitisha Kampeni Team kwa mtu nje ya Mgombea na Chama chake. Vinginevyo, ni dhahiri hapa siyo tu wamefanya bahati mbaya bali wamefanya kwa makusudi kabisa kwa lengo la kudhibiti siyo tu Kampeni Team bali pia kupitia Kampeni Team hizo mikakati yote ya Kampeni ya Wagombea. Hii ni kinyume na dhana ya Demokrasia na ni Tanzania tu ndiyo itakuwa na Sheria ya namna hiyo duniani. Anayefahamu mfano mwingine atumwagie hapa.
Mwanasheria Mkuu ameendelea kupotosha jamii, kwa kutumia utaalamu wake. Nimekaa Bungeni, ni mara ya kwanza jambo kubwa kuingizwa kwenye sheria, na rudia "Kinyemela". Mapambano kuhusu jambo hili ndio kwanza yameaanza, mpaka tutakapopata haki zetu. Ukondoo huu, na kutokufanya utafiti wa kina na au kukubali kila kitu ndio umetufikisha hapa tulipofika. Safari hii tumezinduka na Mwanasheria Mkuu ajue hivyo.

 
Jasusi,
Salaam kutoka Johannesburg. Kwa bahati mbaya wakati Mwanasheria Mkuu alipotoa Tafsiri yake, nilikuwa vijijni, na sasa niko nje ya nchi, lakini nimeona nitembelee Jamvi letu ndio nimekutana na hoja hii. Kutokana na umuhimu wake kwa demokrasia, nimeona nisilaze damu. Hivyo nachangia kama ifuatavyo:-

Hoja yako ni sahihi.i) Hapo ndio kuna utata. Nashukuru kuwa Mwanasheria Mkuu anakiri kuwa "kifungu cha 7(3) kiliongezwa".. Kwa wale wenye kumbukumbu ya Hansard, Kauli ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Zima (Full House Committee- yaani Bunge inapokaa kama Kamati wakati wa kupitisha kifungu kwa kifungu), ni kuwa Tafsiri hiyo iwekwe kwenye "Definition". Kifungu cha (3) siyo Definition. Hivyo ni dhahiri kuwa Serikali kwa kuweka kifungu cha 7(3) imekwenda kinyume kabisa na maelekezo ya wazi na dhahiri ya Kamati ya Bunge zima. ii) Kama nilivyoeleza awali, kilichokuwa kikijadiliwa ni katikakipengele cha 7 ni "Vikundi vya Sanaa. Kampeni Team imetokea wapi katika kifungu hiki iii) Hata kama ilikuwa lazima kukiingiza, je ilikuwa lazima waondoe mamlaka ya kuamua nani awe kwenye Kampeni Team kutoka kwa mgombea na chama chake na kuyahamisha mamlaka hayo kwa Serikali ( je kutakuwa na fair play ground- wakati wanaopewa mamlaka hayo wanajulikana kuwa makada wa Chama Tawala?).
 
Buchanan,
Sahihi kabisa. Namshukuru sana aliyeweka Nukuu ya Hansard kwenye Jamvi. Hoja yangu ya msingi ni kuwa " wapi katika mjadala wote uliokuwepo kwenye Kamati ya Bunge zima suala la "Approving Authority" acha kujadiliwa, hata kutajwa na yeyote kati ya wabunge waliokuwa wakichangia hoja hiyo? Hii ndio hoja, na kwa msngi huo ndio maana nimesema kuwa Mwanasheria Mkuu amepotosha ukweli, kwa sababu yeyote anayoijua yeye. Nadhani wana JF wote watapata nafasi ya kuipitia kumbukumbu hiyo ya Hansard, na watajadili kwa kina hali hii inayotia mashaka,

 
WildCard,
Kama hoja ni kumwamini "AG" kwa kuwa ni mtu "Makini" basi hatuna sababu ya kuwa na Bunge. Kwanini tupoteze fedha na muda mwingi kuwa na Bunge wakati tuna mtu makini tunayemwamini? Nadhani ni hoja dhaifu sana. Sina hakika kama umefuatilia mjadala wote, na kama umeielewa vizuri sheria hii, dhan ya Tume ya Taifa ya uchaguzi umeitoa wapi?

Buchanan,Approval itoke wapi sasa? Ujue Tume yetu ya Taifa ya Uchaguzi haina maofisa wake katika ngazi yoyote ile ya chini kama mkoa, wilaya, jimbo au kata. Tumwamini AG wetu. Ni mtu makini sana ingawa sio malaika.
 

Dr. Slaa.. labda niongeze kuelewesha tatizo la serikali kwenye hili. Kwenye kesi ya wagombea binafsi mojawapo ya sababu za rufaa ni madai ya serikali kuwa Mahakama imejipa madaraka ya Bunge ya kutunga sheria kwa kitendo chake cha kufuta kipengele cha Katiba kinacholazimisha wagombea kuwa wa vyama vya siasa. Wanasema hili ni jambo kubwa na kuwa chombo pekee cha kutunga sheria ni Bunge na hivyo mahakama ingeweza kutoa hukumu bila kuashiria uwepo wa sheria mpya (yaani kuruhusu wagombea binafsi kabla ya uchaguzi huu mkuu).

Sasa kama hili ni kweli (kwamba chombo pekee cha kutunga sheria ni bunge), serikali hiyo hiyo inakuja na sheria yenye vipengele ambavyo havikujadiliwa wala kupitishwa na bunge na kwa maneneno ya AG vimeongezwa na jopo la wataalamu (ambao si wabunge ni wa serikali). Kwa maneno mengine, nguvu ambayo serikali inaikatalia mahakama kwenye suala la mgombea binafsi inajipa yenyewe kwenye suala la sheria ya gharama za uchaguzi. Hiki kinaitwa "double standard"..
 
Hapa kilichobaki ni kwenda Mahakamani tu, MPAKA KIELEWEKE!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…