Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
OFISI YA PETER COLMORE NA ALLY SYKES DAR ES SALAAM 1960s
Kuandika historia ya wafanyabiashara hawa wawili Ally Sykes na Peter Colmore unahitaji kutoa kitabu kizima.
Mimi nimewajua baba zangu hawa katika umri mdogo sana.
Baba zangu hawa mmoja Mwingereza na mwingine Mwafrika na wote hawa wakaja kuwa sehemu ya maisha yangu miaka mingi sana katika ujana wangu.
Nakumbuka kama jana vile siku baba kanichukua ofisini kwa Ally Sykes Mtaa wa Lindi mwisho unapokaribia Mtaa wa Nkrumah.
Ofisi hii ilikuwa nyuma ya International Hotel hoteli nzuri ya kuvutia wakati ule.
Ofisi ya Ally Sykes ni hiyo katika picha ya kwanza.
Mandhari ya ofisi hii imebadilika sana kuelekea ufujaji nilipofika pale Jumapili iliyopita baada ya kuiona zaidi ya miaka 50 iliyopita.
Nyumba hii ilikuwa imesimama peke yake.
Hicho kibanda kilichojengwa mbele ya nyumba hiyo ya gorofa moja kilikuwa hakipo.
Hiki kibanda kimechafua muonekano wa hiyo nyumba na maeneo yanayozunguka nyumba hiyo.
Sehemu nzima hapo haipendezi kama nilivyokuwa naifahamu miaka ile kwani baba alipanga nyumba moja jirani na ofisi hii ya Ally Sykes.
Kuishi sehemu hii kunipelekea kupajua vyema na ilikuwa sehemu wakiishi Magoa wengi na ukipita nje ya nyumba zao utasikia miziki ya Kizungu.
Hutomsikia Mohamed Raffi, Mukesh, Lata Mangeshkar au Asha Bhosle waimbaji nguli wa Kihindi enzi zile.
Nyimbo nilizokuwa nazisikia kutoka nyumba hizi nazikumbuka hadi leo - "Roses Are Red," ya Jim Reeves "Young World," ya Ricky Nelson na "Thank You Girl," ya The Beatles.
Kwa mara ya kwanza niliona kiyoyozi katika ofisi hii ya Peter Colmore na Ally Sykes.
Ofisi hii ya kupendeza ilikuwa na busati lililofunika sakafu ya chumba kizima na kulikuwa na tape recorder kubwa ya "spools," nyakati hizo cassette zilikuwa bado.
Muziki laini ulikuwa unatoka katika chombo hicho.
Nilitamani baba asimalize mazungumzo na Ally Sykes ili nibakie mle ndani nikipigwa na ubaridi na muziki mtamu.
Sasa ngoja nimlete Peter Colmore kwa kifupi sana.
Mara ya kwanza kumuona Peter Colmore ilikuwa hapo mtaani tulipokuwa tunakaa.
Mbali na hii ofisi yake na Ally Sykes, Peter Colmore alikuwa na makazi ya kudumu ndani ya International Hotel Annex na mlango wa chumba chake kulikuwa na "plaque," yenye jina lake.
Vyumba vingine vya jirani havikuwa na kitu kama hicho.
Hii ilinidhihirishia ingawa katika akili ya kitoto kuwa huyu Mzungu alikuwa mtu mkubwa.
Picha ya pili hapo chini ni International Hotel Annex ambapo Peter Colmore alikuwa na makazi yake.
Mkabala na jengo hili ilikuwa International Hotel yenyewe.
Katika hoteli hii mwaka wa 1965 Hamza Aziz alimweka Ali Migeyo baada ya kupewa amri na Rais akamtoe kizuizini Jela ya Ukonga alikokuwa amefungwa.
Hamza Aziz alimkuta Migeyo hana nguo za kuvaa ikabidi are jee mjini amnumulie nguo kwanza amletee kisha ndiyo amweke hoteli.
Ali Migeyo alikuwa anaapishwa siku ya pili Ukumbi wa Karimjee kuwa mbunge.
Ofisi kuu ya Peter Colmore ya kampuni yake High Fidelity Productions ilikuwa Nairobi.
Nitakuja kujua historia ya kampuni hii miaka mingi baadae na mambo makubwa iliyofanya kuanzia uandishi wa vitabu, kurekodi muziki wa wana muziki wakubwa wa Afrika ya Mashariki kama Mwenda Jean Bosco, Eduardo Masengo, Frank Humplink hadi kutoa matangazo ya biashara radioni.
Matangazo haya yakawa maarufu Afrika ya Mashariki yote mfano tangazo la "Aspro ni Dawa ya Kweli."
Kampuni hii ilikuwa ikiwakilisha makampuni makubwa ya biashara na Colmore alipohamia Tanganyika alimchukua Ally Sykes kama mshirika na akanunua hiyo nyumba na kuifanya ofisi yake.
Lakini itapita miaka mingi ndipo nitakuja kufungukiwa na mengi katika historia ya Tanganyika na watu walioitengeneza historia hii na Allah atanijaalia kuwajua watu hawa vyema na kwa karibu sana.
Hii imenisaidia sana kutambua mengi ambayo si wengi wanayajua ya hasad, chuki, wivu na roho mbaya zilizokithiri.
Haya yatapelekea kuharibika historia yote ya TANU na harakati za kudai uhuru.
Ally Sykes alinambia kwa kinywa chake kuwa Peter Colmore ndiye aliyemtajirisha na kumfunza biashara.
Nilipokwenda Nairobi kuonana na Peter Colmore wakati mimi na Ally Sykes tunajaribu kuandika maisha yake na Peter Colmore wakati wa Vita Kuu ya Pili Vya Dunia (1939 - 1945) nilimweleza nini rafiki yake kanieleza kuhusu yeye.
Peter Colmore na yeye akaniambia yake.
Akaniambia kuwa yeye anamshukuru Mungu kuwa maisha yake yamekuwa na manufaa kwa binadamu mwenzake.
Colmore akaniambia kuwa Ally Sykes ndiye aliyeleta fedha nyingi sana katika kampuni kwa kuwa hakupata hata siku moja kushindwa kutimiza wajibu wake.
Kila kazi aliyompa aliifanya kwa juhudi kubwa.
Moja ya kazi ambayo nimeishuhudia kwa jicho langu ni uandishi wa kitabu cha historia ya Tanganyika mwandishi akiwa Lady Judith Listowel mwaka wa 1963 aliyeandika, "The Making of Tanganyika."
Ally Sykes alinionyesha barua alizokuwa akiandikiana na mwanamama huyu wa Kiingereza mke wa Balozi wa Uingereza Accra.
Listowel alimshukuru sana Ally Sykes kwa kumsaidia kuonana na wazalendo viongozi waliopigania uhuru wa Tanganyika.
Lakini taratibu hali ya hewa ilichafuka.
Colmore alinambia ilimsikitisha sana kuona kuwa kuneemeka kwa Ally Sykes katika biashara hili ilimtengenezea maadui ndani ya TANU na serikali.
Uadui huu ulienea hadi kwake.
Peter Colmore aliamua kuondoka na kurudi kwao Kenya na akamuuzia Ally Sykes ile nyumba iliyokuwa ofisi yao.
Haukupita muda serikali ikataifisha nyumba hii na Ally Sykes akawa haeshimiki tena kama muasisi na mfadhili wa TANU bali ni mmoja katika mabepari wanyonyaji.
Hapakuwa na tofauti kati ya Ally Sykes na Peter Colmore.
Ally Sykes na Peter Colmore walikutana Nairobi mwaka wa 1942 ndani ya duka la kuuza vifaa vya muziki la Assanand wote wakiwa wamevaa uniform za KAR.
Ally Sykes alikuwa katika mafunzo ya vita kabla hajakwenda kupigana Burma.
Umri wake ulikuwa miaka 16 na alikuwa katoroka kwao kujiunga na jeshi.
(Baba alihadithia kuwa Ally Sykes alipokuwa katoroka haonekani kwao, mtu wa kwanza kufuatwa na Mzee Kleist kuulizwa alikuwa yeye).
Colmore alishangazwa na Ally Sykes Mswahili kutoka Tanganyika jinsi alivyokuwa na ulimi mwepesi wa kuzungumza Kiingereza.
Udugu wao ulianza hapo na walibaki marafiki hadi Colmore alipofariki mwaka wa 2004.
Ukitaka kuuona mkono wa Peter Colmore katika kuifadhili TANU mtafute kwa Ally Sykes.
Mwaka wa 1958 Ally Sykes alimpeleka Peter Colmore kuonana na Nyerere nyumbani kwake Magomeni.
Uhuru ulipopatikana mwaka wa 1961 Peter Colmore alialikwa kwenye sherehe za uhuru na alihudhuria.
Mwili wa Peter Colmore ulichomwa moto na Ally Sykes alihudhuria maziko haya ya rafiki yake Nairobi.
Ally Sykes aliporudi kutoka mazikoni ndipo aliponipigia simu Tanga kunitaarifu kifo cha Peter Colmore.
Nilikaa kitako na Ally Sykes tukaandika taazia ya Peter Colmore na ikachapwa na The East African.
Picha: Peter Colmore na Ally Sykes Paris 1963, Peter Colmore na Mwandishi Muthaiga, Nairobi 1995.